[ad_1]
Malumbano makali ya ugavana Kitui kati ya Malombe na Kiema
NA RICHARD MUNGUTI
MALUMBANO ya Ugavana wa Kitui yamekumba chama cha Wiper ambapo mzozo unatokota kati ya aliyekuwa Balozi Kiema Kilonzo na Gavana wa zamani Dkt Julius Malombe.
Bw Kilonzo anaomba jopo la kuamua mizozo ya vyama vya kisiasa (PDDT) lizime Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ili isichapishe jina la Dkt Malombe kuwa mwaniaji wa ugavana Kitui akidai hakuna uteuzi uliofanywa.
Bw Kiema anadai wakazi wa Kitui hawakupewa fursa ya kumchagua mpeperushaji bendera ya chama hicho kuwania kiti cha Ugavana Kitui.
Kesi hiyo imeratibishwa kuwa ya dharura.
PDDT imemwamuru wakili Erick Mutua awakabidhi washtakiwa nakala za kesi ili wajibu katika muda wa siku tatu.
Katika kesi hiyo Bw Kiema anayewakilishwa na Bw Mutua amekishtaki chama cha Wiper, IEBC na Malombe.
Kiema anapinga uamuzi wa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka wa kumteua moja kwa moja Bw Malombe kupambana na Gavana Charity Ngilu katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022
Mnamo 2017 Ngilu alimbwaga Malombe na kushinda ugavana Kitui.
Akipinga ushindi wa Bi Ngilu, Dkt Malombe alimshtaki Ngilu lakini mahakama kuu ikatupilia mbali kesi ya Malombe na kuratibisha ushindi wa Ngilu kuwa ni wa halali.
Bw Kiema anaumezea mate Ugavana Kitui.
Katika kesi aliyowasilisha, Bw Kiema anaomba chama cha Wiper kishurutishwe kufanya uteuzi kamili ili kuwapa fursa wapigakura kumteua mwaniaji ugavana wanayemtaka.
Kesi ilikuwa imeratibiwa kusikilizwa Mei 3.
[ad_2]
Source link