Connect with us

General News

Mama wa umri wa miaka 40, wanawe wang’aa KCSE – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mama wa umri wa miaka 40, wanawe wang’aa KCSE – Taifa Leo

Mama wa umri wa miaka 40, wanawe wang’aa KCSE

NA MANASE OTSIALO

MAMA mwenye umri wa miaka 40 kutoka kaunti ya Mandera amepata alama ya B- katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (KCSE) yaliyotolewa Jumamosi na Waziri wa Elimu George Magoha.

Bi Sabriya Ismail Ahmed ambaye alifanya mtihani huo katika shule ya upili ya New Life katika Kaunti Ndogo ya Banisa, pia alifanya mtihani huo pamoja na wanawe wawili, wa kike na kiume, waliopata gredi ya B.

“Nilikatiza masomo katika shule ya upili ya Qubaa iliyoko kaunti ya Mombasa kutokana na ukosefu wa karo na nikaolewa. Lakini hiyo haikuvunja hamu yangu ya kukwea ngazi kimasomo,” akasema mama huyo wa watoto sita.

“Niliamua kurejea shuleni na nikaweza kujisajiliwa kwa mtihani wa KCSE katika Shule ya Upili ya New Light. Nilikuwa nikishirikiana a watoto wangu kudurusu masomo katika harakati za kujiandaa kwa KCSE ya 2021. Ni furaha yangu kwamba sote tuliandikisha matokeo mazuri,” akaambia Taifa Leo, kwenye mahojiano kwa njia ya simu.

Binti yake kwa jia Zeinab Kusse Abdi alipata gredi ya B lakini mwanawe wa kiume Mohamed Amin hakuwa amefichua gredi yake tulipokuwa tukienda mitambo.

Hata hivyo, Amin alishikilia kuwa amepata gredi ambayo itamwezesha kuitwa katika mojawapo ya vyuo vikuu vya umma nchini.