Connect with us

General News

Man-City wapepeta Brighton na kurejea kileleni mwa jedwali la EPL – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Man-City wapepeta Brighton na kurejea kileleni mwa jedwali la EPL – Taifa Leo

Man-City wapepeta Brighton na kurejea kileleni mwa jedwali la EPL

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City waliwaruka Liverpool na kurejea tena kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kufunga mabao matatu katika kipindi cha pili na kupepeta Brighton 3-0 mnamo Jumatano usiku ugani Etihad.

Baada ya kulemewa na Brighton ya kocha Graham Potter katika kipindi cha kwanza, Man-City walifungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Riyad Mahrez aliyeshirikiana vilivyo na Kevin de Bruyne kunako dakika ya 53.

De Bruyne alichangia pia bao la tatu ambalo Man-City walifungiwa na Bernardo Silva mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya Phil Foden kupachika wavuni goli la pili katika dakika ya 65.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City sasa wanadhibiti kilele cha jedwali la EPL kwa alama 77, moja pekee mbele ya Liverpool ambao pia wametandaza michuano 32. Zimesalia mechi sita kabla ya kampeni za EPL kukamilika rasmi muhula huu.

Man-City wana ulazima wa kushinda kila mojawapo ya mechi hizo, wakianza na Watford mnamo Aprili 23 ugani Etihad, ili kuhifadhi taji la EPL. Pambano dhidi ya Brighton lilikuwa la 250 kwa Mahrez ambaye ni raia wa Algeria kusakata katika EPL. Bao lake lilisaidia Guardiola kushinda mechi yake ya 250 katika soka ya EPL. Mechi hiyo ilikuwa ya nane kati ya tisa zilizopita kwa Brighton kupoteza dhidi ya Man-City ligini. Isitoshe, Brighton hawajashinda mchuano wowote dhidi ya Man-City ugenini katika historia ya EPL.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending