Connect with us

General News

Man-United wamvizia Valverde kuwa kocha mshikilizi wanapozidi kumshawishi Pochettino – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Man-United wamvizia Valverde kuwa kocha mshikilizi wanapozidi kumshawishi Pochettino – Taifa Leo

Man-United wamvizia Valverde kuwa kocha mshikilizi wanapozidi kumshawishi Pochettino

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United wamemzungumzia kocha wa zamani wa Barcelona, Ernesto Valverde kuhusu uwezekano wa kudhibiti mikoba yao kwa muda wanapoendelea kumsaka kocha mpya atakayeajiriwa kwa mkataba wa kudumu.

Valverde, 57, anapigiwa upatu kushikilia mikoba ya Man-United waliomtimua Ole Gunnar Solskjaer kwa sababu ya matokeo duni.

Mpango wa kumwendea Valverde ni zao la mikakati ya kuwapa Man-United muda zaidi wa kuafikiana na mkufunzi wa Paris Saint-Germain (PSG), Mauricio Pochettino ambaye nafasi yake jijini Paris inatarajiwa kutwaliwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane.

Kazi ya mwisho kwa Valverde katika ulingo wa ukocha ni kudhibiti mikoba ya Barcelona aliowaongoza kutwaa mataji mawili mfululizo ya La Liga na ubingwa wa Copa del Rey kabla ya kupigwa kalamu Januari 2020.

Aliwahi pia kujitwalia mataji matatu ya Ligi Kuu ya Ugiriki akidhibiti mikoba ya Olympiakos kabla ya kuaminiwa fursa za kunoa Espanyol, Valencia na Athletic Bilbao aliowatia makali katika zaidi ya michuano 300 kwa awamu mbili tofauti.

Licha ya kutowahi kunoa kikosi chochote cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Valverde anajivunia umilisi mkubwa wa Kiingereza. Tangu Solskjaer atimuliwe, mikoba ya Man-United kwa sasa inadhibitiwa na kiungo wao wa zamani, Michael Carrick.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending