General News
Mapinduzi yalivyotishia demokrasia Afrika 2021 – Taifa Leo
Published
4 years agoon
By
Taifa Leo [ad_1]

Mapinduzi yalivyotishia demokrasia Afrika 2021
Na BENSON MATHEKA
MWAKA wa 2021 ulishuhudia wanajeshi wakipindua serikali za nchi kadhaa na kuzua hofu ya kuangamizwa kwa demokrasia iliyokuwa imeshika kasi na kunawiri barani Afrika.
Mnamo Septemba 5 Kanali Mamady Doumbouya alijitokeza katika runinga ya serikali ya Guinea na kutangaza kwamba alikuwa amepindua serikali ya raia.
Hii ilikuwa baada ya kuongoza vikosi vya kijeshi kuvamia makazi ya Rais Alpha Conde, aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.
Kuchaguliwa kwa Conde kulichukuliwa kuwa mwanzo mpya katika nchi hiyo baada ya kutawaliwa kimabavu na wanajeshi kwa miongo mingi.
Wanajeshi hao walisambaza picha za Conde akiketi kwenye sofa bila kuvalia viatu huku wakimzingira wakishika silaha kali.Mapinduzi ya Guinea hayakuwa ya pekee mwaka wa 2021 kusini mwa jangwa la Sahara. Kulikuwa na mapinduzi manne ya wanajeshi kunyakua mamlaka barani Afrika.
Mnamo Oktoba, wanajeshi wa Sudan waliwakamata na kuwazuilia viongozi wa kiraia. Hatua hiyo ilijiri mwezi mmoja baada ya mamlaka nchini humo kutangaza kwamba jaribio la mapinduzi lilikuwa limezimwa.
Mkuu wa Majeshi ya Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitwaa mamlaka Oktoba 25 na kumzuilia waziri mkuu Abdalla Hamdok ambaye awali walikuwa wamekubaliana kushirikiana kuongoza nchi.
Jenerali Abdel Fattah al- Burhan alimrejesha Hamdok mamlakani kufuatia shinikizo kutoka kwa raia waliozidisha maandamano na presha kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Hata hivyo, jeshi lingali na ushawishi mkubwa katika nchi hiyo likiwa linathibiti siasa.Mnamo Mei, wanajeshi wa Mali walipindua serikali kwa mara ya pili ndani ya miezi kumi.Mapinduzi ya Mali yalitokea wakati raia walikuwa wakiandamana dhidi ya serikali ya Rais Ibrahim Boubacar Keita, ambayo wapinzani waliilaumu kwa ufisadi, ubaguzi, upendeleo na kukosa kukabiliana vilivyo na mzozo wa usalama unaoendelea kudorora katika nchi hiyo.
Katika mapinduzi ya Mali na Sudan, viongozi wa kijeshi walitumia mbinu sawa kunyakua mamlaka. Wanajeshi waliopindua serikali ya kiraia ya Mali chini ya uongozi wa Kanali Assimi Goita awali waliahidi kuunda serikali ya mpito ya mseto wa kijeshi na raia.
Hii ilikuwa baada ya mapinduzi ya kwanza Agosti 2020 ambapo waliahidi kurejesha uongozi wa kiraia kumaliza kipindi cha mpito.
Lakini mnamo Mei, Goita alimkamata na kumtupa jela rais wa kiraia na waziri mkuu wa baraza la mpito akiwalaumu kwa kubadilisha mawaziri ambapo wanajeshi wawili walipokonywa uwaziri na nafasi zao zikajazwa na wanasiasa.
Goita alisema hakushauriwa kabla ya mabadiliko hayo kufanywa, akanyakua mamlaka na kujitangaza rais huku akiahidi uchaguzi mkuu Februari 2022 ambao wadadisi wanasema ni vigumu kufanyika.
KATIBA
Nchini Mali, Jenerali Mahamat Idriss Deby alinyakua mamlaka kwa kufutilia mbali Katiba na kuvunja bunge kufuatia kifo cha baba yake, Rais Idris Deby.
Mapinduzi ya kijeshi yaliyokuwa yamechacha barani Afrika kati ya 1960 na 2000 yameanza kurejea jambo lililomfanya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuyalaani vikali.
Wadadisi wanasema kwamba kuchipuka kwa mapinduzi ya kijeshi barani Afrika, kunachangiwa pakubwa na mataifa na mabwenyenye ya kigeni ambayo yanalinda maslahi yao, masuala ya kindani yanayokasirisha umma kama vile ufisadi, ukosefu wa usalama na utawala mbaya.
Kwa mfano, mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea yalijiri baada ya malalamishi na maandamano dhidi ya hatua ya Conde kuondoa mihula miwili ya rais kuhudumu.
Hii ilimfanya Kanali Doumbouya kutetea hatua yake ya kupindua serikali akidai kuwa umaskini na ufisadi ulisukuma kikosi spesheli cha kijeshi kuchukua hatua.
Wadadisi wanasema kuwa viongozi wanachangia mapinduzi ya kijeshi kwa kuvuruga Katiba, kuondoa mihula ya marais kuhudumu na kuvuruga mchakato wa uchaguzi jambo linalofanya umma kuunga wanajeshi kwa kuwataka waingilie kati kuokoa nchi zao.
Ryan Cummings, Mkurugenzi wa kampuni ya Signal Risk, anasema kwamba wanajeshi hujitwika nafasi ya mwokozi na kutumia malalamishi ya raia ‘kuhalalisha’ hatua yao ya kunyakua mamlaka kinyume cha Katiba.
Japo Muungano wa Afrika na Mashirika ya Kimaeneo kama vile Jumuiya ya Uchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) husimamisha uhusiano na nchi ambazo wanajeshi wanatwaa mamlaka, wataalamu wanasema kwamba hazina nguvu ya kushinikiza viongozi wa kijeshi wanaopindua serikali kurejesha utawala wa kiraia.
Aidha, wanalaumu jamii ya kimataifa kwa kutochukua msimamo mkali dhidi ya viongozi wa kijeshi wanaopindua serikali za kiraia barani Afrika.
“Hatua hii inazua hofu ya kuendelea kwa hali hii na kuhatarisha demokrasia ambayo ilisitisha umwagikaji wa damu uliosababishwa na utawala wa kimabavu wa wanajeshi na madikteta barani Afrika kati ya 1960 na 2000,” asema David Kinuthia, mtaalamu wa utatuzi wa mitafaruku.
Anasema nchi zenye nguvu kama China na Amerika zina sera ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika mradi tu zimejitolea kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uchumi.
“Urusi imekuwa ikipanua ushawishi wake kisiasa na kijeshi barani Afrika kwa kuunga viongozi wanaopindua serikali kama Goita wa Mali na al-Burhan wa Sudan,” asema.
Hofu imetanda kuwa ubabe wa mataifa yenye nguvu ulimwenguni kibiashara na kijeshi, unaweza kuchangia mapinduzi zaidi barani Afrika ikisemekana kuwa kundi hatari la Wagner linalohusishwa na Urusi limetuma mamluki katika nchi zinazokumbwa na mizozo kama Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mali na Libya.
MAKALA MAALUM: Uunganishaji haramu wa stima waweka wakazi…
[ad_2]
Source link
Comments
You may like
Wantam Protests Hit Ugunja as CS Opiyo Wandayi Loses Support, Youths Invite DCP Led by Rigathi Gachagua
South Sudan at the Brink: How Corruption Tightens Its Grip on a Rare Working Institution
Chepterit Comes Alive During SportyBet Kenya Gifts Motorbike to Loyal Fans
Nest Lounge Narok Under Scrutiny as KRG The Don Shooting Incident Triggers Government Silence and Maasai Community Outcry
Why the Sh323.8 Billion Kenya US Health Agreement Is Raising Data Privacy Questions
Betty Bayo’s Mother Seeks DPP Inquest Over Daughter’s Death
Ugunja Women Cry Foul After MP Appointments Snub Them Despite Campaign Support
KSh4M Serve! SportyBet Kenya Title Sponsors for Kipchumba Karori Eldoret International Volleyball Tournament
Shadrack Maritim Resurfaces in Uganda After Two-Month Disappearance
