Connect with us

General News

Marjan ateuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Marjan ateuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC – Taifa Leo

Marjan ateuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC

NA CHARLES WASONGA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imemteua rasmi Marjan Hussein Marjan kuwa Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ezra Chiloba.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jumatano, Machi 9, 2022 alisema kuwa Bw Marjan ndiye aliibuka bora zaidi baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuajiri mshikilizi wa afisi hiyo.

Afisa huyo ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu Afisa Mkuu Mtendaji tangu Oktoba 28, 2018 Bw Chiloba alipopigwa kalamu, kwa mienendo mibaya.

Marjan ni miongoni mwa watu wanne waliorodheshwa kwa mahojiano kujaza nafasi hiyo ni; Nancy Wanjiku, Joel Zephania Okeyo na George Michugu. Jumla ya watu 500 walituma maombi ya kutaka wateuliwa kwa wadhifa huo.

Awali, Bw Marjan amekuwa akihudumu kama Naibu Afisa Mkuu Mtendaji.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending