[ad_1]
Matajiri nchini wahofia kuachia kizazi kipya mali yao
NA MARY WANGARI
URITHI wa mali umetajwa miongoni mwa hofu kuu ya matajiri nchini Kenya, ripoti mpya inasema.
Kulingana na Ripoti mpya kuhusu Utajiri iliyotolewa jana na shirika la Knight Frank, idadi kubwa ya mabilionea nchini Kenya kwa asilimia 31 wameelezea wasiwasi wao kuhusu kurithisha mali yao kwa kizazi kipya.
Idadi hii ni kubwa mno ikilinganishwa na asilimia 20 ya matajiri duniani wanaohofia kurithisha mali yao.
“Kuachia utajiri kwa kizazi kipya ni wakati muhimu mno kwa mabilionea kote duniani kwa kuwa usimamizi duni wa michakato ya urithi unaweza ukasababisha utajiri kudidimia upesi.
“Nchini Kenya, hata hivyo, huku kukiwa na ushahidi kila mara wa mizozo na hata kesi zinazodumu kortini kwa muda mrefu, tishio hilo linachochewa na kiwango cha changamoto katika kurahisisha au kuharakisha matokeo ya mizozo kama hiyo,” alifafanua Mkurugenzi wa Knight Frank, Ben Woodhams.
Utafiti huo pia ulitaja masuala mengineyo yanayohofiwa na mabil – ionea kama tishio kwa utajiri wao huku mabadiliko ya hali ya anga yakiwa mstari wa mbele kwa (asilimia 84) ikilinganishwa na asilimia 53 duniani ikifuatiwa na aina mpya ya virusi vya Covid-19 kwa asilimia 81 ikilinganishwa na asilimia 66 duniani.
Usawa katika masoko ya kimataifa kwa asilimia 69 ikilinganishwa na asilimia 10 duniani, mifumo ya usambazaji bidhaa kwa asilimia 63 ikilinganishwa 55 duniani pamoja na mabadiliko ya utandawazi kwa asilimia 56 ikilinganishwa na asilimia 40 duniani.
Utafiti huo ulionyesha kuwa idadi ya matajiri wakuu duniani iliongezeka kwa watu 52,000 zaidi ambao ni sawa na asilimia 9.3 ambapo idadi ya matajiri barani Afrika ilipungua pakubwa mwaka jana hasa kuhusiana na janga la Covid-19.
Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi kubwa ya matajiri nchini wana mipango ya kupata uraia mpya kama sehemu ya kuwekeza huku wengi wao wakipanga kutuma maombi ya kupata pasipoti ya pili au uraia mpya kwa lengo la kuwekeza zaidi, elimu na kupata huduma za afya.
Next article
Karata ya kuteua manaibu gavana sasa yafichuka
[ad_2]
Source link