Connect with us

General News

Matiang’i ausifu ukumbi wa kisasa wa Mwai Kibaki Convention Centre MKU – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Matiang’i ausifu ukumbi wa kisasa wa Mwai Kibaki Convention Centre MKU – Taifa Leo

Matiang’i ausifu ukumbi wa kisasa wa Mwai Kibaki Convention Centre MKU

Na LAWRENCE ONGARO

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i, amekisifu Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) kwa kujitambulisha katika ramani ya dunia.

Alizuru chuo hicho mnamo Alhamisi ambapo alisifu ukumbi mpya uliozinduliwa hivi majuzi katika chuo hicho wa Mwai Kibaki Convention Centre, akiutaja kama wa hadhi ya kimataifa.

Alisema ukumbi huo una umuhimu wake wa kipekee kwa sababu unatumika kuandaa makongamano yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa.

“Ukumbi huo ni muhimu kwa sababu unaweza kutumiwa kwa hafla za maombi na pia kwa makongamano tofauti. Kwa hivyo, ni hatua kubwa iliyochukuliwa na MKU,” alisema Dkt Matiang’i.

Alisema amepata habari ya kwamba chuo hicho kiliandaa kongamano kubwa la amani kuhusu maswala ya uchaguzi.

“Ninawahimiza washika dau wengine popote walipo wawe mstari wa mbele kutumia ukumbi huo kama njia ya kumtunuka sifa Rais wa Tatu wa Kenya Bw Mwai Kibaki ambaye alimpokeza Rais Uhuru Kenyatta kijiti cha uongozi,” alisema Dkt Matiang’i.

Alisema wakati Rais mstaafu Mwai Kibaki alitoa hotuba yake katika Chuo Kicha Makerere, alivitaka vyuo vikuu katika bara la Afrika viwe na mwelekeo wao ili kuboresha masomo vyuoni.

Ukumbi wa Mwai Kibali Convention Centre umeendesha makongamano mengi ya kibiashara.

Sehemu ya ukumbi wa kisasa wa Mwai Kibaki Convention Centre katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) mjini Thika. Picha/ Lawrence Ongaro

Kongamano lingine la YUNUS Social Business Summit linatarajiwa kuendelea kwa wiki moja na litawaunganisha washiriki 10,000 kupitia mitandao ya kisasa.

Waziri vilevile lipongeza MKU kwa kupiga hatua ya kusomesha wanafunzi wa sheria wapatao 30.

Chuo hicho pia kimepongezwa kwa kushirikiana na hospitali kuu ya Thika Level 5, huku kikijenga jumba la kuhifadhi maiti ambalo ni sehemu ya uapanuzi kutoka nafasi ya maiti 40 hapo awali na sasa kuna nafasi ya maiti 1,000 kwa wakati mmoja.

Tayari wanafunzi 40,000 wamepitia chuoni humo kwa kujisimamia kimasomo wenyewe.

Inaelezwa kuwa kila mwaka wanafunzi wapatao 10,000 hufuzu kwa kutunukwa shahada mbalimbali.

Mwanzilishi wa chuo hicho Profesa Simon Gicharu, alisema ukumbi wa Mwai Kibaki Convention Centre ni muhimu kwa kujumuisha vikundi tofauti kutoka pembe zote za dunia.

Alimsifu Rais mstaafu Mwai Kibali kwa kukipandisha hadhi chuo hicho na hivyo kupokea cheti maalum cha kujisimamia rasmi.

“Wanafunzi wengi waliopitia MKU wamepata mwelekeo na mapokezi mema katika sehemu wanazokwenda kutokana na masomo yanayotambulika kimataifa,” alisema Prof Gicharu.

Prof Gicharu aliusifu ukumbi huo kwa kuongoza makongamano tofauti ya kimataifa huku ukisifika kwa usimamizi wake mzuri.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending