[ad_1]
Mauaji ya watu 11 yazua hofu Isiolo
NA WAREMU WAIRIMU
VIONGOZI wa Kaunti ya Isiolo wamelalamikia utovu wa usalama eneo hilo huku visa vya uvamizi wa ujangili vikiendelea kuongezeka baada ya watu 11 kuuawa ndani ya siku mbili.
Mnamo Alhamisi, watu watano kutoka Wajir waliuawa katika eneo la Lokale baada ya mapigano kati ya jamii mbili kuzuka kwenye mpaka wa Isiolo na Wajir.
Wakati wa uvamizi huo, watu wawili waliokuwa wakiendeshwa kwenye bodaboda walipigwa risasi na majangili katika tukio hilo la Jumatatu usiku Wajir Magharibi.
Miili ya wawili hao, ambao walikuwa wakielekea Kom, ilipatikana imetupwa kando ya barabara saa nne usiku ikiwa na majeraha. Jamii hasimu nayo ilijibu mashambulizi hayo na kusababisha vifo vya watu sita na mmoja akajeruhiwa vibaya.
Mnamo Jumatano, wanaume wawili walipigwa risasi na majambazi wanaodaiwa walitoka Samburu. Wawili hao walikuwa wakilisha mifugo eneo la Attan kabla ya dereva wa lori lililokuwa limebeba mchanga kuuawa mnamo Alhamisi asubuhi.
Ripoti ya polisi ilionyesha kuwa uvamizi uliotokea Merti ulilenga kuondoa baadhi ya jamii kutoka kwa ardhi yao.
Next article
IEBC kuchunguza madai ya Ruto kuwa kuna njama ya wizi wa…
[ad_2]
Source link