Connect with us

General News

Mawaziri wapya wateuliwa mahali pa walioingia siasani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mawaziri wapya wateuliwa mahali pa walioingia siasani – Taifa Leo

Mawaziri wapya wateuliwa mahali pa walioingia siasani

NA SIAGO CECE

SERIKALI ya Kaunti ya Kwale imeanza kufanya mabadiliko ya wizara baada ya sehemu ya baraza la mawaziri kujiuzulu kuwania viti vya kisiasa katika uchaguzi ujao.

Katika Kaunti ya Kwale, Gavana Salim Mvurya amefanya mabadiliko katika Wizara ya Utamaduni na Elimu baada ya mawaziri kujiuzulu.

Miongoni mwa walioondoka ni Katibu wa kaunti hiyo, Bw Martin Mwaro ambaye anamezea mate kiti cha ubunge cha Magarini, Kaunti ya Kilifi.

Wengine ni wa – ziri wa Elimu Mangale Chiforomondo anayelenga kiti cha Lungalunga, na mwenzake wa huduma za kijamii na usimamizi wa vipaji Ramadhan Bungale (Matuga).

Afisa wa Utumishi wa Umma na Utawala katika kaunti, Bi Sylvia Chidodo ndiye ameteuliwa kuchukua nafasi ya katibu wa kaunti.