Connect with us

General News

Mbunge ajitetea kuhusu matumizi ya fedha za NG-CDF – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbunge ajitetea kuhusu matumizi ya fedha za NG-CDF – Taifa Leo

Mbunge ajitetea kuhusu matumizi ya fedha za NG-CDF

Na GEORGE ODIWUOR

MBUNGE wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo ametetea usimamizi wake dhidi ya madai ya matumizi mabaya ya fedha, baada ya ripoti ya ukaguzi kuhusu mali ya umma kuonyesha jinsi baadhi ya wabunge wameshindwa kuwajibikia pesa za walipa ushuru.

Katika ripoti yake ya ukaguzi wa bajeti 2018/2019, Mkaguzi Mkuu Nancy Gathungu, alisema wabunge kadhaa hawawezi kufafanua jinsi mamilioni ya pesa za walipa ushuru zilivyotumika katika Hazina ya Ustawishaji wa Maeneobunge (NG-CDF).

Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa Bungeni, inaonyesha jinsi wabunge walivyotumia vibaya pesa za basari na matumizi mengine bila ithibati ya jinsi hela hizo zilivyotumiwa.Katika eneo la Suba Kaskazini, usimamizi wa Bi Odhiambo, uliripotiwa kutumia fedha hizo katika miradi ambayo ilipaswa kutekelezwa na serikali ya Kaunti ya Homa Bay.

Miradi hiyo inayozua utata ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kilomita mbili hadi Shule ya Msingi ya Wakondo uliogharimu Sh3 milioni.Aidha, Bi Odhiambo anasemekana kutumia Sh 3.9 milioni kujenga barabara nyingine ya kilomita 2.6 hadi katika Shule za Msingi za Nyamaji Kisaka na Ndhuru.

‘Sheria imesema wazi kuhusu majukumu yangu na yale ya serikali ya kaunti,” alisema