Connect with us

General News

Mbunge aomba TSC iongeze walimu shuleni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbunge aomba TSC iongeze walimu shuleni – Taifa Leo

Mbunge aomba TSC iongeze walimu shuleni

Na ALEX KALAMA

MBUNGE wa Ganze Teddy Mwambire ameitaka serikali iongeze walimu katika shule za sehemu hiyo.

Akizungumza na Taifa Leo kwa njia ya simu, Bw Mwambire alisema kwamba wazazi wameachiwa mzigo mkubwa wa kuajiri walimu kwa sababu ya uhaba.

‘Hata baada ya kujizatiti zaidi kama eneo bunge la Ganze kuweza kuelimisha walimu wengi zaidi hususani wa shule za msingi bado kuna upungufu mkubwa wa walimu,” alisema.

Kukiwa na upungufu kama hivi ni kumaanisha kwamba wazazi ni wajukumike waweze kuajiri walimu wengine.

“Ni kumaanisha bado ni mzigo mkubwa unapatiwa wazazi. Kwa hivyo tunarai serikali kuu iweze kuleta mipango mipya waajiri walimu wengi zaidi,’ alisema Bw Mwambire.

Hata hivyo mbunge huyo alisema changamoto za utovu wa nidhamu shuleni zimesababishwa na ukosefu wa walimu wa kutosha.

Aidha alisema idadi ya walimu wakutosha inapaswa kuoana na ile ya wanafunzi ili elimu iweze kuimarika zaidi.

‘Tunalaumu walimu wengi kusema kwamba shule watoto hawana nidhamu mpaka wengine wanachoma shule ila ni kwa sababu wanafunzi ni wengi walimu ni wachache. Umiliki wa wanafunzi kwa mfano 500 kwa walimu 8 inakuwa ni ngumu zaidi.

“Ni lazima idadi ya walimu imbatane na idadi ya wanafunzi ndio kutakuwa na nafasi ya kuweza kuwambia kwa ukaribu. Kwa sababu wanafunzi wengine wanaweza kuwa na matatizo na hawapati nafasi ya kuwasiliana na mwalimu,’ alisema Bw Mwambire.