Njaa: Mbunge aomba wahisani wawasaidie wakazi na chakula
Na MAUREEN ONGALA
MBUNGE wa Magarini, Bw Michael Kingi, ametoa wito kwa wahisani kusaidia wakazi wa Kilifi wanaoendelea kukumbwa na njaa.
Bw Kingi alisema chakula cha msaada kutoka serikali kuu na ile ya kaunti hakitoshi idadi kubwa ya wakazi ambao wameathirika.Alisema hayo alipoungana na kampuni ya Kensalt kutoa msaada wa bidhaa za chakula kwa wakazi wa eneobunge hilo.