Connect with us

General News

Mbunge apokea baraka za maaskofu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbunge apokea baraka za maaskofu – Taifa Leo

Mbunge apokea baraka za maaskofu

Na WINNIE ONYANDO

MBUNGE wa Westlands, Tim Wanyonyi (pichani) amepokea baraka kutoka kwa maaskofu wa makanisa mbalimbali nchini kabla ya kuanzisha rasmi kampeni yake ya kuwania kiti cha ugavana Kaunti ya Nairobi.

Akizungumza Jumatatu katika eneo la United Kenya Club, Nairobi, Bw Wanyonyi alisema kuwa yuko tayari kuwania kiti hicho na kuleta maendeleo katika kaunti hiyo.

“Niko tayari kuwania kiti cha ugavana. Baada ya kupokea baraka kutoka kwa maaskofu, najua nitashinda. Nitaendelea kuwatumikia wakazi wote wa Nairobi jinsi ambavyo nimewatumikia watu wa eneobunge langu. Nitaleta maendeleo katika kaunti hii,” akasema Bw Wanyonyi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending