Connect with us

General News

Mbunge Lempurkel jela mwaka mmoja kavu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbunge Lempurkel jela mwaka mmoja kavu – Taifa Leo

Mbunge Lempurkel jela mwaka mmoja kavu

Na RICHARD MUNGUTI

MUSTAKABALI wa kisiasa wa aliyekuwa Mbunge wa Laikipia Kaskazini Mathew Lempurkel haujulikani baada ya kusukumwa jela mwaka mmoja bila faini kwa kumchapa na kumjeruhi mbunge Sarah Korere, miaka mitano iliyopita.

Iwapo Mahakama Kuu haitabatilisha kifungo hicho, Lempurkel hataruhusiwa kisheria kuwania kiti cha ubunge, useneta au ugavana.

Lempurkel alifungwa bila faini na Hakimu Mwandamizi Hellen Onkwani aliyempata na hatia ya kumchapa na kumuumiza Bi Korere ndani ya afisi ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa ndani, marehemu Jenerali Joseph Nkaissery mnamo Novemba 21, 2016.

Akipitisha hukumu hiyo, Bi Onkwani alisema ushahidi uliowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) umethibitisha Bw Lempurkel alitenda uhalifu huo.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Bw James Gachoka uliwaita mashahidi 10.

“Baada ya kutilia maanani ushahidi wote wa upande wa mashtaka na ule wa Lempurkel, hii mahakama imefikia uamuzi kwamba, mshtakiwa alifanya makosa kumtandika mateke na masumbwi Bi Korere na kumsababishia majeraha,” alisema Bi Onkwani.

Hakimu alisema ingawa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza, yeye ni kiongozi na mbunge wa zamani anayeelewa dhuluma dhidi ya wanawake na watoto haziruhusiwi kamwe.

“Kwa vile unajua ukweli dhuluma dhidi ya wanawake na watoto haziruhusiwi kisheria, hii mahakama imekupata na hatia jinsi ulivyoshtakiwa,” alisema Bi Onkwani.

Akaendelea, “Utatumikia kifungo cha mwaka mmoja bila faini.”

Upande wa mashtaka uliwaita mashahidi 10 ikiwa ni pamoja na daktari wa idara ya polisi aliyethibitisha Bi Korere alijeruhiwa.

Mnamo Septemba 8, mbunge huyo alikamatwa kutokana na kile mshirikishi wa shughuli za serikali ya kitaifa katika eneo la Rift Valley George Natembeya alisema ni mchango wa mbunge huyo katika kuendeleza visa vya ujangili katika Kaunti ya Laikipia.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending