Connect with us

General News

Mbwembwe tele katika sherehe ya mwisho ya Uhuru – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbwembwe tele katika sherehe ya mwisho ya Uhuru – Taifa Leo

Mbwembwe tele katika sherehe ya mwisho ya Uhuru

NA CHARLES WASONGA

ILIKUWA ni shamrashamra Jumatano katika sherehe ya 59 ya Madaraka Dei iliyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi.

Hiyo ndio ilikuwa sherehe ya mwisho ya kitaifa kuongozwa na Rais Kenyatta ambaye anastaafu baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Wakenya walianza kuwasili katika bustani hiyo iliyoko kando ya barabara ya Lang’ata saa kumi na mbili alfajiri .

Usalama uliimarishwa ndani na nje ya bustani hiyo huku wananchi na wageni waalikwa wakikaguliwa na maafisa wa usalama kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Vile vile, wananchi walizuiliwa kuingia katika uwanja huo wakiwa wamebeba chupa za maji au wakivalia kofia na mavazi yenye rangi zinazoashiria muegemeo fulani wa kisiasa.

Kwa mara ya kwanza vikosi vya jeshi la Kenya vilionyesho zana za kivita za kisasa.