Mcheshi matata aliyekuwa akifanya kazi na Radio Maisha Francis Munyao almaarufu MCA Tricky ametimka kutoka kituo hicho kinachomilikiwa na Kampuni ya Standard Group.
Mchekeshaji MCA Tricky agura Radio Maisha, akimbia kuichukua nafasi ya Jalang’o Milele FM Picha: Nation Source: UGC
Kulingana na vyanzo ndani ya kampuni hiyo ambavyo vimezungumza na TUKO.co.ke moja kwa moja kupitoa simu, ni kweli mchekeshaji huyo yupo njiani kuelekea Milele FM inayomilikiwa na Mediamax.
Vyanzo hivyo vimeendelea kusema kuwa, Tricky ataichukua afasi iliyochwa wazi na mchekeshaji mwenzake Felix Oduor almaarufu Jalang’o aliyekuwa akifanya kazi na Alex Mwakideu kipindi cha asubuhi kwa jina Milele Breakfast.