Connect with us

Entertainment

Mchekeshaji maarufu Othuol Othuol aruhusiwa kuondoka hospitalini

Published

on

– Othuol Othuol alipatikana na uvimbe kwenye ubongo na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wakati wowote

– Mchekeshaji huyo amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Kenyatta kwa muda wa wiki moja

– Madaktari wamemruhusu kuondoka hospitalini ila atakuwa akifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu kila baada ya siku tatu kwa muda wa miezi 3

– Othuol amekuwa akisumbuliwa na magonjwa kadhaa ikiwemo kifuu kikuu

Mchekeshaji maarufu wa kipindi cha Churchill Show Othuol Othuol ameruhusiwa kuondoka hospitali baada ya kulazwa kwa siku kadhaa.

 

Othuol Othuol

Othuol amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta ambapo madaktari waligundua kwamba yuko na uvimbe kwenye ubongo.

Kabla ya kulazwa Kenyatta iliripotiwa kuwa mchekeshaji huyo alizirai akiwa nyumbani kwake na alikimbizwa katika hospitali moja mtaani Kitengela.

Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa Kenyan Digest, Othuol atakuwa akienda hospitali kila baada ya siku tatu kwa muda wa miezi mitatu kwa ajili ya ukaguzi wa kimatibabu.

Aidha, Meneja wa Churchill Show Ken Waudo amesema msanii huyo yuko katika hali nzuri na amewashukuru wasanii wengine kwa kuingilia kati na kuchanga fedha zilizogharamia matibabu yake.

Hata hivyo, haijabainika ni lini atafanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe huo

Othuol amekuwa akisumbuka na magonjwa tangu mwaka wa 2019 ambapo alipatikana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Comments

comments

Facebook

Trending