Connect with us

General News

Mgomo wa matrela waingia siku ya nne – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mgomo wa matrela waingia siku ya nne – Taifa Leo

Mgomo wa matrela waingia siku ya nne

Na BRIAN OJAMAA

Madereva wa malori ya kusafirisha mizigo kwenye barabara ya Mombasa –Malaba wamegoma wakilalamikia ada za Sh3,600 wanazotozwa na serikali ya Uganda kupimwa virusi vya corona.

Walilalama kuwa ada hizo mpya za kupimwa corona katika kituo cha mpaka wa Kenya na Uganda cha Malaba ilikuwa ya juu mno kwao kuimudu.

Walisema kwamba ni Uganda pekee wanakotakiwa kuitishwa ada kupimwa ilhali wanapimwa bila malipo Kenya na Rwanda.

Madereva hao wamesababisha msongamano mkubwa wa zaidi ya kilomota 80 kutokaMalaba hadi Kanduyi kaunti ya Bungoma.