Connect with us

General News

Mhasibu anayejua thamani ya ndege maridadi jijini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mhasibu anayejua thamani ya ndege maridadi jijini – Taifa Leo

Mhasibu anayejua thamani ya ndege maridadi jijini

Na SAMMY WAWERU

SEKTA ya kilimo na ufugaji ni mojawapo ya zinazoendelea kunoga, licha ya changamoto zinazoizingira.

Inazidi kupata washirika, hasa baada ya Kenya kukumbwa na janga la corona. Kulingana na takwimu za wizara, idadi ya wakulima na wafugaji nchini imeongezeka, wengi wa wahanga wa Covid-19 hususan waliopoteza nafasi za ajira na kufunga biashara zao, wakigeukia shughuli za kilimo na ufugaji.

Peter Kimani, ni mmoja wa walioathirika baada ya kupoteza kazi jijini Nairobi. Alikuwa mhasibu katika kampuni moja jijini na baada ya kuchujwa, aligeuza biashara ya ufugaji wa ndege maridadi kuwa afisi yake ya kila siku.NKimani aliingilia ufugaji wa nyuni 2016, kama mbinu ya kujipa pato la ziada.

“Nilianza na mayai 200 ya kanga, yaliyoatamiwa na kuangua vifaranga,” asema, akidokeza kila yai aliuziwa Sh50. Miaka sita baada ya kuingilia ufugaji wa ndege wa umaridadi jijini, ana kila sababu ya kutabasamu. Ni miongoni mwa wafugaji na wazalishaji hodari wa mazao ya nyuni.

Mtaa wa Umoja, jijini Nairobi, na wenye shughuli chungu nzima za kibiashara, kuanzia uuzaji wa bidhaa za kula, mazao mabichi ya shambani, mavazi, na uchukuzi, kati ya nyinginezo, katika makazi ya kukodi Kimani ameyagawanya kusitiri mradi wake.

Ana vizimba kadhaa, ambavyo ni boma la bata aina ya Pekins, Rouen, Silkie bantams – kuku, Egyptian runners na kuku wa kienyeji. Vilevile, mfugaji huyu ambaye ni baba wa watoto wawili, ana kanga. Ni wa madoadoa meusi na meupe na wengine wa rangi nyeupe pekee. Hali kadhalika, Kimani hufuga bata bukini, bata mzinga na njiwa.

Mfugaji Peter Kimani akilisha kuku aina ya bantams, anaowafugia eneo Umoja, Nairobi…Picha/ SAMMY WAWERU

Unapotua katika mazingira yake, utakaribishwa na sauti tofauti za ndege hao walioyarembesha ajabu. Mseto wa muwiko wa nyuni wa kiume unahinikiza hewa. Isitoshe, rangi yao maridadi itakuvutia, utatamani kushinda nao mchana kutwa.

“Hulka zao ndio chanzo changu cha mapato,” Kimani aelezea. Vizimba amevigawanya kusitiri kila aina ya ndege, na pia kwa mujibu wa umri. Nyuma ya nyumba anayoishi, yapo makazi ya ‘ghorofa’ na bustani ya ndege kuchezea. Mbele katika egesho la gari, ana kizimba kingine. Ni mpangilio anaohoji ukiigwa na wakazi wenza maeneo ya mijini, watajipa njia mbadala kusukuma gurudumu la maisha.

“Wanachohitaji, ni kuwa na ari. Si lazima iwe ni shughuli za ufugaji, kilimo cha matunda ya thamani kama vile stroberi na mboga kinawezekana,” afafanua, akihimiza wapangaji mijini haswa wenye nyumba zilizo na bustani kukumbatia wazo hilo. Margaret Njeri, ni mfugaji wa ndege wa umaridadi na kuku wa kienyeji walioboreshwa eneo la Mwihoko, Ruiru, Kaunti ya Kiambu, kiungani mwa jiji la Nairobi.

“Muhimu ni kupanga nafasi iliyopo, na kuigeuza kuwa chanzo cha mapato,” Njeri asema. Mfugaji huyu ana mamia ya ndege na kuku, biashara yake ikiwa ni ya mayai. Lengo la Peter Kimani ni kuangua mayai, na kuuza ndege wa kurembesha mazingira. “Wengi wa wanunuzi, wamekumbatia nyuni kama wanyama vipenzi (pets) kuyafanya mazingira yao kuwa maridadi,” adokeza.

Huuza ndege wake kwa pea, jogoo na mtetea (kiume na kike). Licha ya kufanikisha ufugaji jijini, anasema Wizara ya Afya ilipoweka marufuku ya ama kuingia au kutoka Nairobi na viunga vyake 2020, alikadiria hasara kubwa. Hata ingawa amri hiyo iliyotekelezwa kusaidia kudhibiti msambao wa virusi vya corona iliondolewa, Kimani analalamikia kulazimika kuuza pea ya ndege waliopaswa kugharimu zaidi ya Sh5, 000, chini ya Sh1, 000.

“Wengi sikuwa na budi kuuza Sh500,” adokeza, akikumbuka hasara aliyokadiria. Hata hivyo, anasema biashara yake imeanza kuamka baada ya serikali kulegeza kamba sheria na mikakati kuzuia corona. Hutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kufanya matangazo ya mauzo.

Mfugaji Peter Kimani akiwa katika kizimba cha kuku aina ya bantams, anaowafuga Umoja, Nairobi…Picha/ SAMMY WAWERU

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending