[ad_1]
Mhubiri ashtakiwa kwa madai ya kuchafua mtoto
Na JOSEPH NDUNDA
MHUBIRI jana alishtakiwa katika Mahakama ya Kibera kwa madai ya kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka sita, mtaani Kawangware, Nairobi.
Askofu Michael Shikutansi Masinde wa Kanisa la Africa Green Cross Apostle, anadaiwa kumnajisi mtoto huyo ndani ya nyumba yao mnamo Machi 25.
Mahakama ilielezwa kuwa mtoto alikuwa akicheza nje ya nyumba ya wazazi wake, alipomhadaa msichana huyo kwa kumpa peremende kabla ya kumtendea kitendo hicho.
Baadaye alimpa pesa ili amnyamazishe ila akaonekana akiondoka nyumbani kwa mshukiwa akiwa na maumivu. Watoto waliomwona, walipiga nduru zilizovutia umati ambao ulimfikisha hadi kituo cha polisi.
Mtoto huyo alifikishwa hadi hospitali moja jijini ambako alitibiwa kisha akajaza fomu ya matibabu.
Mshukiwa huyo alikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Kibera, William Tulele.
Aliomba mahakama pia imwonee huruma kwa sababu yeye ni baba wa watoto sita ambao wanamtegemea.
Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 na kesi hiyo itatajwa Aprili 20 mwaka huu.
Next article
Msimamizi akosoa miradi hewa kwenye kaunti
[ad_2]
Source link