– Mhubiir Mugweru aligonga vichwa vya habari baada ya mmoja wa washirika kutoa ushuhuda wa penzi tamu la pasta
– Mugweru alikuwa amemchukua na kumgeuza mpenziwe licha ya kuwa alikuwa mama aliyeolewa
– Bwanake mama huyo aliteta kwa askofu kutovunja ndoa yake lakini gari la mapenzi ya wawili hao lilikuwa tayari limeondoka
Pasta wa Juja aliyemchukua mmoja wa washirika wake na kumfanya mpenziwe amepatikana ameuawa.
Askofu Francis Mugweru wa kanisa la Joy Springs Soul-winning Worship Centre alipatikana akiwa ameuawa katika eneo la Kiganjo, Juja, mita chache kutokakwake.
Familia ya askofu Francis Mugweru katika kito cha polisi kutafuta haki kwa jamaa wao. Picha: Star Source: UGC
“Tunaomba haki ifanyike kwa ndugu yetu na baba wetu wa kiroho. Polisi wanafaa kuhakikisha waliotenda haya wamewajibishwa. Nilikutana na mwili huo saa chache nikienda kazini lakini sikujua ni ndugu yangu.
Baadaye ndio nilipigiwa simu na kuambiwakuwa ndiye aliyekuwa ameuawa,” Njuguna alisema.
Askofu Mugweru aligonga vichwa vya habari 2013 baada ya kuachana na mkewe Agnes Wangivi na badala yake akahepa na mmoja wa kondoo wake kanisani aliyemgeuza na kuwa mke.
Washirika wa kanisa la Joy Springs Juja alipokuwa akihudumu askofu Francis Mugweru. Picha: Star Source: UGC
Mshirika huyo alikuwa ni mke wa John Kanyua, ambaye pia alikuwa ni mshirika wake na rafiki wa kutoka utotoni.
Mapenzi katika ya askofu huyo na mkewe Kanyua yalishika mizizi na wote kuacha boma zao.
Ni kisa ambacho kilizua hisia kali kutoka kwa Kanyua na licha ya kumpembeleza askofu asivunje ndoa yake, mkewe alikataa kurudi akisema penzi la askofu Mugweru lilikuwa tamu zaidi.