[ad_1]
Middlebrough yadengua Man-United kwenye Kombe la FA kupitia penalti
Na MASHIRIKA
MANCHESTER United waliaga kampeni za Kombe la FA msimu huu baada ya Middlesbrough kuwadengua kwenye raundi ya nne ya kipute hicho kwa penalti 8-7 mnamo Ijumaa usiku uwanjani Old Trafford.
Mshindi wa mechi hiyo aliamuliwa kupitia penalti baada ya pande zote mbili kusajili sare ya 1-1 kufikia mwisho wa muda wa kawaida.
Chipukizi Anthony Elanga alipaisha mkwaju wake kwa upande wa Man-United na kuwapa mashabiki 9,000 wa Middlesbrough kila sababu ya kuondoka uwanjani wakitabasamu.
Droo ya raundi ya tano ya Kombe la FA itafanyika Jumapili ya Februari 6, 2022 baada ya Liverpool kualika Cardiff City, Leicester City kumenyana na Nottingham Forest na AFC Bournemouth kuchuana na Boreham Wood katika michuano mingine ya raundi ya nne mnamo Februari 5, 2022.
Middlesbrough sasa hawajapigwa katika mechi 11 zilizopita kwenye mashindano yote na wanapigiwa upatu wa kutamalaki kampeni za Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) na kurejea kwenye EPL msimu ujao wa 2022-23.
Hii ni mara yao ya pili baada ya kukutana na kikosi cha EPL mara 11 kwenye Kombe la FA ambapo wamesonga mbele kwenye kivumbi hicho. Mara ya mwisho ilikuwa 2015 walipozamisha Manchester City kwa mabao 2-0 ugani Etihad.
Fedheha zaidi kwa Man-United ni kwamba waliochangia kudenguliwa kwao kwenye Kombe la FA mnamo Ijumaa ni chipukizi wao wa zamani – Duncan Watmore, Matt Crooks na Paddy McNair.
Licha ya Man-United kutamalaki mchezo na kumiliki asilimia kubwa ya mpira, Cristiano Ronaldo alipiga nje penalti katika kipindi cha kwanza nao Bruno Fernandes na Jadon Sancho wakapoteza nafasi nyingi za wazi langoni mwa Middlesbrough.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link