Connect with us

General News

Midume hii ya KU inalenga kuteka handiboli ya kanda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Midume hii ya KU inalenga kuteka handiboli ya kanda – Taifa Leo

Midume hii ya KU inalenga kuteka handiboli ya kanda

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya wanaume ya Chuo cha Kenyatta (KU) ya mchezo wa handiboli, inasadiki kuwa itajikaza mithili ya mchwa ili kuhifadhi taji la kitaifa baina ya vyuo vikuu nchini (KUSA) muhula huu.

KU ni kati ya vikosi ambavyo hutoa upinzani mkali kwenye mechi za Ligi Kuu ya Handiboli (KHF). Chini ya nahodha Samuel Katuva, wasomi hao wanajivunia kutawazwa mabingwa wa KUSA msimu uliopita.

Pia ni miongoni mwa vikosi ambavyo vimekuza chipukizi kibao waliosajiliwa na klabu zingine za ligi nchini.“Jinsi nimetazama wachezaji wangu, wana uwezo wa kufanya vyema kwenye mashindano tofauti nchini,” alihoji kocha Victor Luvale, ambaye husaidiana nao Catherine Cherotich na Robert Osano.

SUPER CUPKU wakati iliwika kwenye mechi za ligi kuu ilikuwa msimu 2013/14, ikiibuka nambari mbili na kufuzu kushiriki kinyang’anyiro cha Super Cup. Kwenye mechi za KUSA, wanafahamu wapinzani wao wamejipanga kuwakabili kwa udi na uvumba, ingawa kocha Luvale asema pia “tumepanga wachezaji wetu vizuri na tayari kuteremsha ushindani wa kufa mtu.

” FAINALI ZA KUSA Katika michuano ya KUSA kanda ya Nairobi msimu uliokamilika Oktoba, KU ilimaliza kileleni na kufuzu kwa fainali za kitaifa zilizopigiwa uga wa Chuo Kikuu cha Eldoret (UoE).

Waliwazaba wasomi wenzao Jomo Kenyatta (JKUAT) mabao 26-19. Sasa shabaha yao imevuka mipaka na mkufunzi huyo adokeza kuwa “pia nataka tufuzu mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati hivi karibuni.”

Katika nusu-fainali, KU ilivuna 26-23 dhidi ya Mt Kenya (MKU) wakati JKUAT ikinyuka UoE.Kwenye utangulizi wa mechi za ligi ya KUSA Kanda ya Nairobi muhula huu leo Jumamosi, wasomi wa KU wamepangwa kufungua kampeni zake dhidi ya GRESTA.

Kocha Catherine Cherotich anasema anatamani sana kuona KU chini ya uongozi wao ikimaliza kati ya nne bora kwenye kampeni za ligi kuu ndani ya miaka mitano ijayo. ”Pia ninataka tufuzu kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati hivi karibuni,” kocha huyo alisema na kuongeza kuwa itakuwa furaha kwake akiongoza kikosi hicho kushiriki kipute hicho.

KU inajivunia kuchangia mchezaji mmoja Titus Kipruto kuteuliwa katika timu ya taifa mwaka 2019. ?Idadi ya wachezaji waliowahi kchezea KU walipokuwa wanafunzi chuoni humo na kujiunga na timu zingine inajumuisha:Dennis Magoiya, Victor Luvale, Charles Malema, Titus Kipruto, Dennis Munjera na Patrick Njagi wote Black Mamba.

Clinton Maiko, Nicholas Okore, William Malui, Snox Collins na Brian Wakukha wote Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini (NCPB). Pia wapo Shel Kuya na Bethuel Kiptoo wa Kahawa na Buccaneers mtawalia.

KU inajumuisha:Samuel Katuva (nahodha), Morgan Simiyu (naibu wa nahodha), Julius Chiunda, Dickson Wanyama, Fresnel Khisa, Donald Idaho, Onesmus Aron, Amos Keter na Isaac Nyongesa. Pia wapo Phelix Ongoro, Harrison Mwadali, Willis Musembi, Isaiah Wafula na Wenceslaus Ochieng.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending