Connect with us

General News

Miedema aweka rekodi ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Uingereza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Miedema aweka rekodi ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Uingereza – Taifa Leo

Miedema aweka rekodi ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Uingereza

Na MASHIRIKA

VIVIANNE Miedema aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kuchangia mabao 100 katika Ligi ya Soka ya Wanawake nchini Uingereza (WSL) alipoongoza waajiri wake Arsenal kukomoa Birmingham 4-2 mnamo Jumapili.

Miedema ambaye pia anaongoza orodha ya wafungaji bora katika historia ya WSL, anajivunia mabao 10 hadi kufikia sasa msimu huu. Alifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Birmingham ugani Meadow Park. Rafaelle Souza alifungulia Arsenal ukurasa wa mabao kabla ya Beth Mead kufanya mambo kuwa 3-0.

Ingawa Libby Smith na Lucy Quinn walirejesha Birmingham mchezoni, Caitlin Foord alizamisha kabisa chombo cha wageni wao na kusaidia Arsenal kufungua pengo la alama nane kileleni mwa jedwali la WSL.

Arsenal walinyanyua taji la WSL mara ya mwisho mnamo 2019 na wanapigiwa upatu wa kutawazwa mabingwa msimu huu japo wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Chelsea wanaonolewa na Emma Hayes.

Kati ya mabao 100 ambayo Miedema amechangia katika WSL, 70 ni yale amepachika wavuni huku akihusika moja kwa moja katika magoli 30 mengine ambayo yamefungwa na wenzake tangu ajiunge na Arsenal mnamo 2017.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO