Connect with us

General News

Milly Nafula wa A- apata fursa kuingia chuo kikuu baada ya zaidi ya miaka 15 ya mahangaiko – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Milly Nafula wa A- apata fursa kuingia chuo kikuu baada ya zaidi ya miaka 15 ya mahangaiko – Taifa Leo

Milly Nafula wa A- apata fursa kuingia chuo kikuu baada ya zaidi ya miaka 15 ya mahangaiko

Na LAWRENCE ONGARO

MAMA wa watoto wawili aliyepata alama ya A- katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) na kukosa kujiunga na chuo kikuu, amepata ufadhili wa masomo.

Bi Milly Nafula aliyekosa nafasi ya kuingia chuoni miaka 15 iliyopita, mnamo mwishoni mwa wiki jana alipata ufadhili wa kujiunga na Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) ili kutimiza ndoto yake ya kuendelea na masomo.

Mwanzilishi wa chuo hicho Profesa Simon Gicharu, alieleza kuwa chuo hicho kimetenga Sh3.5 milioni za kumfadhili mwanamke huyo ili akamilishe masomo yake ya udaktari aliyokamia kufanya wakati huo wa awali.

Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika kitengo cha chuo hicho kilichoko mjini Kitale cha Africa College of Medical and Health Science.

“Ufadhili huo utamwezesha mwanamke huyo kuafikia lengo lake la kuendelea na masomo yake aliyotamani zaidi ya miaka 15 iliyopita,” alifafanua Prof Gicharu.

Naye Bi Nafula alisema ya kwamba hatua iliyochukuliwa na MKU ni ya kupongezwa na yeye kwa upande wake atafanya juhudi kuona ya kwamba anafanya bidii masomoni na kufanikiwa.

“Ninajua niko na kibarua kikubwa mbele yangu ikizingatiwa kwamba nimechukua muda mrefu bila kuendelea na masomo. Lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ninaelewa nitafanikiwa,” alisema Bi Nafula.

Wakazi wa kijiji chao eneo la Magharibi mwa Kenya, wamepongeza MKU kwa kuchukua hatua hiyo ya kumsaidia mwana wao aendelee na masomo yake ya juu.

Bi Nafula alieleza kuwa atafanya juhudi kuona ya kwamba amefaulu kwenye mitihani yake ili atakapopata jukumu la kuhudumia wananchi aendeshe kazi hiyo kwa bidii na unyenyekevu.

” Ninajua wananchi wanangoja kuona matunda ya jasho langu nami ninawahakikishia kuwa nitafanya lolote niwezalo kuona ya kwamba ninafanikiwa hadi niwe daktari kamili wa kutibu wagonjwa. Najua hayo yote yanataka kujitolea na kuwa na bidii,” alijitetea Bi Nafula.