Connect with us

General News

Mipango ya mazishi ya mamake Waititu yaendelea – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mipango ya mazishi ya mamake Waititu yaendelea – Taifa Leo

TANZIA: Mipango ya mazishi ya mamake Waititu yaendelea

Na WINNIE ONYANDO

MPANGO wa kumzika mama wa aliyekuwa gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu aliyeaga dunia Jumapili unaendelea.

Bw Waititu almaarufu Baba Yao alisema kuwa mamake, Monicah Njeri Waititu, 93, alikufa akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan Nairobi.

Bi Njeri, ambaye ameacha watoto saba, huenda akazikwa wiki hii Limuru.

“Nimempoteza rafiki mkubwa na mama yangu mpendwa ambaye nilikuwa nikimtazamia kila wakati. Amekuwa mgonjwa kwa muda ila sasa ametuacha,” akasema Bw Waititu.

Kwa upande wake, Naibu wa Rais, Dkt William Ruto alituma rambirambi zake kwa familia ya Bw Waititu huku akimtaja Bi Njeri kama mpenda amani, mwenye maarifa na mkarimu.

“Naungana na Wakenya kumwomboleza Bi Monicah Waititu. Tumempoteza mama ambaye alikuwa mkarimu na mpenda amani,” akaomboleza Dkt Ruto.