[ad_1]
TUSIJE TUKASAHAU: Miradi ya serikali yafaa kukamilishwa
NA CHARLES WASONGA
WAZIRI wa Fedha Ukur Yatani juzi alisema kuwa serikali inajadiliana na wanakandarasi kwa lengo la kufutilia mbali jumla ya miradi 437 ya miundo msingi iliyoanzishwa miaka ya nyuma.
Bw Yatani alisema hatua hiyo ni kutokana na uhaba wa fedha za kukamilisha miradi hiyo iliyoanzishwa katika utawala huu na ule wa rais mstaafu Mwai Kibaki.
Lakini Bw Yatani alisahau kwamba, mnamo Julai 27, 2018 bosi wake, Rais Uhuru Kenyatta ilipiga marufuku kuanzishwa kwa miradi mipya ya serikali kuu ili rasilimali zote zielekezwe katika kukamilishwa kwa miradi iliyoanzishwa zamani.
Alisema pesa zote ambazo serikali ingepokea kama mikopo kutoka nje zingeelekezwa katika ukamilishwaji wa miradi hiyo kabla ya kuondoka kwake afisini, 2022.
Akiongea na maafisa wakuu wa serikali, akiwemo Waziri Yatani, katika ukumbi wa Jumba la KICC, Nairobi, Rais Kenyatta aliongeza kuwa hatua hiyo itakomesha kile alichotaja kama ubadhirifu wa rasilimali za umma na kukomesha malimbikizi ya madeni yanayodaiwa serikali.
Next article
Kanuni mpya zatoa afueni kwa waliochukua mikopo ya simu
[ad_2]
Source link