– Amina Mude alimuomba msamaha Ben Kitili kwa kuanika ndoa yao kwenye mtandao jamii
– Alitangaza kuwa mtangazaji huyo ndiye mwanamume wake wa ndoto na atasalia kuwa mke wake katika hali yote
– Mama huyo wa watoto wawili alikiri kwamba ni jukumu lake kama mke kumuheshimu mume wake na kumlinda
Katika hali yote iwe kwa magonjwa na afya njema, kwa umaskini na utajiri ni kifo ndicho kitatutenganisha. Hii ndio ahadi ambayo wanandoa huapa kabla ya kuingia katika ndoa.
Mama huyo akiwa mwingi wa majuto kwenye Instagram, alimuomba mume wake radhi hadharani siku chache baada ya kutangaza kuwa walitengana na mwaka mmoja kufuatia harusi yao.
Amina alisema aliongozwa na hasira kupitia njia mbovu na asingelimwaga mtama kwenye kuku wengi.