Connect with us

General News

Mkome sana Kalonzo, Ngilu amuonya Ruto – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mkome sana Kalonzo, Ngilu amuonya Ruto – Taifa Leo

Mkome sana Kalonzo, Ngilu amuonya Ruto

Na BENSON MATHEKA

GAVANA wa Kitui Charity Ngilu amemuonya Naibu Rais William Ruto dhidi ya kumtusi na kumdharau kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.

Bi Ngilu alimtetea vikali Bw Musyoka akisema ni kiongozi wa jamii ya Wakamba na hatakubali Dkt Ruto na washirika wake kumkosea heshima.

Alipozuru Machakos Jumatano wiki hii, Dkt Ruto alidai kwamba ni yeye aliyemwachia Bw Musyoka nafasi ya kuwa makamu wa rais baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

“Nataka kumwambia William Ruto, akome kuwatusi viongozi. Alipozuru Ukambani nilimsikia akimtusi kiongozi wetu Mheshimiwa Stephen Kalonzo Musyoka, kiongozi wa hadhi ya juu, kiongozi wetu asiye na doa, muadilifu na anayeheshimika na hatutakubali hilo,” Bi Ngilu alisema kwenye ujumbe aliochapisha katika anwani zake za mitandao ya kijamii.

Alisema kwamba alikuwa mshirika mkuu katika uchaguzi mkuu wa 2007 na hana habari wadhifa ambao Dkt Ruto alishikilia ambao alidai alimwachia Bw Musyoka.

“Nilishiriki uchaguzi mkuu wa 2007 na sijui ni wadhifa gani ambao Ruto alikuwa nao ambao alimwachia kiongozi wa hadhi ya Bw Musyoka,” alieleza Bi Ngilu.

Kwenye uchaguzi wa 2007 ambao ulifuatiwa na ghasia mbaya katika historia ya Kenya, Dkt Ruto aligombea kiti cha eneobunge la Eldoret Kaskazini kwa tiketi ya chama cha ODM ilhali Bw Musyoka aligombea urais kwa tiketi ya chama cha ODM-Kenya ambacho baadaye alibadilisha jina kuwa Wiper.

Bi Ngilu alimkemea Dkt Ruto kwa kukosea heshima viongozi waliotoa mchango mkubwa kwa nchi hii wakishikilia nyadhifa tofauti.

“Anafaa kujitazama na kung’amua kwamba hata tofauti za umri kati yake na Bw Musyoka hazimruhusu kumtusi kiongozi wetu ambaye sio tu katika kaunti hii, Machakos na Makueni bali pia amekuwa makamu wa rais wa nchi,” alisema.

Alimtaja Bw Musyoka kama kiongozi mwadilifu sana, wa kutegemewa kitaifa na kimataifa na wa kuaminiwa.

“Tofauti kati ya Bw Musyoka na Ruto ni kuwa mmoja ni mwadilifu, Kalonzo ni mwadilifu sana, kiongozi wa kutegemewa na mwaminifu ambaye anatia bidii kuleta amani katika nchi hii, na kwa hivyo ukimlinganisha na mtu kama Ruto ni kama usiku na mchana,” alisema Bi Ngilu ambaye ni mwanachama wa bodi ya kitaifa ya kampeni ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kupitia vuguvugu lake la Azimio la Umoja.

“Kalonzo ni kiongozi mwema tunayemfahamu, mtu asiye na doa, sio mkora, sio jina unalofaa kucheza nalo. Sio kama Ruto, Ruto ana jina gani? Hauwezi kuja Ukambani na kuanza kumtusi kiongozi wetu ilhali umejaa matope,” alisema.

Bi Ngilu ni mmoja wa viongozi wanaomrai Bw Musyoka kuungana na Bw Odinga ili kumshinda Dkt Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Ingawa kwa muda alikuwa akiungana na magavana Alfred Mutua (Machakos) na Kivutha Kibwana (Makueni) kumkosoa Bw Musyoka, siku za hivi ameonekana kulegeza msimamo. dhidi ya makamu rais huyo wa zamani.