Connect with us

General News

Mmiliki wa Chelsea, Abramovich, akabidhi kamati kuu majukumu ya kuendesha kikosi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mmiliki wa Chelsea, Abramovich, akabidhi kamati kuu majukumu ya kuendesha kikosi – Taifa Leo

Mmiliki wa Chelsea, Abramovich, akabidhi kamati kuu majukumu ya kuendesha kikosi

Na MASHIRIKA

MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich, amesema amekabidhi klabu hiyo kwa wanakamati wakuu wa wakfu wa kikosi hicho ambao sasa watasimamia shughuli zote za kuendesha kikosi.

Abramovich ambaye atasalia kuwa mmiliki wa Chelsea, amechukua hatua hiyo kutokana na uvamizi ambao Urusi wametekeleza dhidi ya Ukraine.

Maamuzi hayo pia yanatokea kabla ya Chelsea kupepetana na Liverpool katika fainali ya Carabao Cup usiku wa Februari 27, 2022 ugani Wembley.

“Nimekuwa nikifanya maamuzi kwa ajili ya kuchangia uthabiti wa kikosi cha Chelsea,” akasema bwanyenye huyo.

Chama cha Mashabiki wa Chelsea hata hivyo kimetaka ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi kamati hiyo itakavyoshughulikia uendeshaji wa klabu.

Abramovich ni miongoni mwa Warusi wakwasi zaidi na inaaminika kwamba ana uhusiano wa karibu sana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Chini ya umiliki wa Abramovich, Chelsea wanajivunia kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mara mbili, ufalme wa Europa League mara mbili, League Cup mara tatu, Kombe la FA mara tano na Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mara tano.

Mnamo Agosti 2021, kikosi hicho kilinyanyua taji la Uefa Super Cup na walitwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mnamo Februari 2022 baada ya kukomoa Palmeiras ya Brazil.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending