Connect with us

General News

Montreal anayochezea Wanyama yalima Inter maandalizi ya msimu mpya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Montreal anayochezea Wanyama yalima Inter maandalizi ya msimu mpya – Taifa Leo

Montreal anayochezea Wanyama yalima Inter maandalizi ya msimu mpya

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal ilianza maandalizi ya msimu mpya kwa kulipua wenzao kutoka Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) Inter Miami 2-1 Februari 5.

Wenyeji Inter Miami walitangulia kutetemesha nyavu za Montreal katika kipindi cha kwanza uwanjani DRV PNK kabla ya Motreal kujibu baada ya mapumziko kupitia mabao mawili ya Ivy Brisma.

Montreal itamenyana na Philadelphia Union mnamo Februari 8 na Miami FC mnamo Februari 11 kabla ya kuanza msimu na mechi ya Klabu Bingwa ya Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF) dhidi ya Santos Laguna kutoka Mexico mnamo Februari 16 ugenini.

Vijana wa kocha Wilfried Nancy wataalika Laguna mjini Montreal katika mchuano wa marudiano Februari 23. Mechi dhidi ya Laguna ni za raundi ya 16-bora. Montreal imerejea kwenye Klabu Bingwa baada ya kukosa msimu uliopita.

Mechi ya kwanza ya kiungo mkabaji wa Kenya, Victor Wanyama tangu ajiunge na Montreal kutoka Tottenham Hotspur ilikuwa kwenye Klabu Bingwa dhidi ya Olimpia kutoka Honduras mnamo Machi 10, 2020.

Kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza cha CF Montreal:

James Pantemis (kipa), Zorhan Bassong, Gabriele Corbo, Karifa Yao, Mathieu Choinière, Victor Wanyama, Lassi Lappalainen, Djordje Mihailovic, Ahmed Hamdi, Joaquin Torres, Sunusi Ibrahim.