Connect with us

General News

Moto wateketeza hekta 550 za msitu wa Aberdare kwa siku tatu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Moto wateketeza hekta 550 za msitu wa Aberdare kwa siku tatu – Taifa Leo

Moto wateketeza hekta 550 za msitu wa Aberdare kwa siku tatu

NA MERCY MWENDE

ZAIDI ya hekta 550 za msitu wa Aberdare zimeharibiwa na moto ambao umekuwa ukiwaka tangu Jumamosi usiku.

Moto huo ambao ulianza katika sehemu tano tofauti za msitu umeathiri sehemu ya Kaskazini ya Aberdares katika eneo la Eburru.

Akizungumza na Taifa Leo, Mkuu wa Shirika la Misitu (KFS) katika Eneo la Kati Bw Samuel Ihure

alisema kuwa kufikia Jumatatu asubuhi, maafisa wa Shirika la Wanyamapori (KWS) na KFS bado walikuwa wanapambana na moto mmoja uliosalia.

“Jana (Jumapili), tulizima mioto mitatu na kubakisha miwili; mmoja ulijizima leo asubuhi na ukabaki mmoja ambao sasa tunasaidiwa na wazima moto wa mashirika tofauti ya ulindaji wa mazingira nchini,” akasema Bw Ihure.

Mkurungezi wa Shirika la Mount Kenya Trust

Susie Weeks alieleza kuwa moto huo ulianza katika sehemu ya Moorlands na ulikuwa bado haujasambaa katika maeneo mengine.

Kufikia Jumatatu, wazimamoto 35 walipelekwa katika sehemu hiyo ili kusaidia katika opersheni.

Alilaumu joto jingi na upepo katika majira ya mchana ambayo hufanya vigumu kuzima moto.

“Mwanzoni, kulikuwa na upungufu wa wazimamoto lakini sasa wapo wengi kutoka mashirika tofauti kutusaidia kukabili moto,” akasema.