Connect with us

General News

Mpango wa Ajira Digital kuwezesha vijana kubuni njia za kujipatia mapato mtandaoni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mpango wa Ajira Digital kuwezesha vijana kubuni njia za kujipatia mapato mtandaoni – Taifa Leo

Mpango wa Ajira Digital kuwezesha vijana kubuni njia za kujipatia mapato mtandaoni

Na LEONARD ONYANGO

Ikiwa wewe ni mkulima na haujui jinsi ya kutangaza mazao yako mtandaoni, unaweza kujiunga na mpango wa ‘Ajira Digital’ kujipatia maarifa.

Waziri Msaidizi wa Mawasiliano na Teknolojia (ICT), Maureen Mbaka, anasema kuwa mpango wa Ajira Digital unatoa mafunzo kuhusu namna ya kutangaza biashara, yakiwemo mazao, mitandaoni hivyo kupanua soko.

“Kupitia mpango wa Ajira Digital, vijana wanaweza kunufaika na fursa za kuwaletea mapato kama vile kutafsiri, kuhariri ripoti za utafiti, kuandika makala kati ya kazi nyinginezo,” anasema Bi Mbaka.

Serikali ya Kitaifa kwa ushirikiano na Muungano wa Sekta za Kibinafsi (Kepsa), wiki iliyopita ilizindua mpango wa kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo katika eneo la Nyanza ili kuwapa mafunzo kuhusu namna ya kutangaza bidhaa zao mtandaoni.

Vijana katika maeneo ya Nyanza pia wanaendelea kufunzwa kuhusu jinsi ya kujipatia mapato kutoka mtandaoni.Utafiti uliofanywa hivi majuzi ulibaini kuwa jumla ya vijana milioni 1.2 humu nchini wanajipatia mapato kwa njia ya mtandao.

Serikali inakadiria kuwa kufikia 2024, mitandao itachangia Sh1.4 trilioni kwa mapato ya kitaifa (DGP) kila mwaka, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ajira Digital, Bw Ehud Gachungu.

Mtu anayehitaji kujipatia maarifa kupitia mpango wa Ajira Digtal anapaswa kujisajili kupitia tovuti ya ajiradigital.go.ke.

“Baada ya kujisajili, chagua aina ya mafunzo unayohitaji katika kituo kilicho karibu nawe. Vituo hivyo vimeorodheshwa katika tovuti hiyo,” anasema Bw Gachungu.