[ad_1]
Mpango wa ODM kumpa Ong’era tikiti wazua utata
NA WYCLIFFE NYABERI
Hisia mseto zimeibuka miongoni mwa wafuasi wa chama cha ODM katika Kaunti ya Kisii, kuhusu ni nani anayefaa kupokezwa tikiti ya kuwania uwakilishi wa wanawake kupitia chama hicho cha chungwa.
Hii ni baada ya madai kuibuka jana kuwa uongozi wa chama cha ODM, ulikuwa umeafikia uamuzi wa kumpa mwakilishi wa sasa, Bi Janet Ong’era (kati pichani)tikiti ya moja kwa moja kutetea wadhfa wake kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.
Hii linamaanisha kwamba, wawaniaji wengine zaidi ya wanne waliokuwa wakimezea mate tikiti hiyo watakosa vyama vha kusimama navyo baada ya dirisha la kuhama vyama kufungwa rasmi wikendi iliyopita.
Kambi inayoonekana kusononeka sana na habari hizo ni ile ya aliyekuwa mwanahabari wa redio Bi Dorice Aburi.
Kwenye vikao viwili tofauti vilivyoandaliwa na wafuasi wa Bi Ong’era na Bi Aburi jana mjini Kisii, kila wafuasi walivuta kamba upande wa kwao.
Katika kikao cha kwanza, wafuasi wa Bi Aburi, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho katika kaunti ya Kisii Bw Kerosi Ondieki, walisema wanataka mchujo wa wadhfa huo ufanyike ili wakazi wa Kisii wajichagulie atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Next article
Wawaniaji roho mkononi mchujo wa ODM ukianza
[ad_2]
Source link