Connect with us

General News

Mpishi aliyekula akashindwa kulipa bili ‘April Fools’ Day’ ashtakiwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mpishi aliyekula akashindwa kulipa bili ‘April Fools’ Day’ ashtakiwa – Taifa Leo

Mpishi aliyekula akashindwa kulipa bili ‘April Fools’ Day’ ashtakiwa

NA RICHARD MUNGUTI

MPISHI aliyekula na kunywa Siku ya Wapumbavu Duniani (Aprili 1, 2022) katika hoteli moja ya kifahari na kushindwa kulipa bili ya Sh6,850 ameshtakiwa.

James Simiyu Wafula alikiri kwamba alikula na kunywa bila pesa za kugharimia starehe zake.

Simiyu alichangamkia chakula katika hoteli ya Park Inn Radison Blu iliyoko katika mtaa wa Westlands, Nairobi mnamo Aprili 1, 2022.

Simiyu alikuwa na miadi ya kukutana na mtu mwingine ambaye hakufika hotelini jinsi walivyopanga.

Mahakama ilielezwa kwamba mshtakiwa aliwasili katika hoteli hiyo kwa bodaboda.

Mshtakiwa alimwagiza mwendeshaji pikipiki huyo ajistareheshe na kile moyo wake ulitamani.

Kwa upande wake Simiyu, aliagiza mlo na pombe kali.

Alishindwa kulipa ndipo akapelekwa katika kituo cha polisi na kufunguliwa mashtaka.

Mshtakiwa aliomba msamaha na kusema akipewa muda atalipa.

Hata hivyo hakimu mwandamizi Esther Boke alimweleza mshtakiwa hata akilipa lazima atatozwa faini kwa kuvunja sheria.

Hakimu aliamuru ripoti ya afisa wa urekebishaji tabia iwasilishwe kortini kabla ya hukumu kupitishwa.