Connect with us

General News

Mrithi wa Uhuru kubeba zigo zito – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mrithi wa Uhuru kubeba zigo zito – Taifa Leo

Mrithi wa Uhuru kubeba zigo zito

Na LEONARD ONYANGO

MIRADI iliyokwama, Mfumo wa Elimu ya Ulimilisi (CBC), madeni, ufisadi, ongezeko la idadi ya vijana wasio na ajira ni miongoni mwa mizigo mizito ambayo Rais Uhuru Kenyatta atamwachia mrithi wake mwaka 2022.

Wadadisi wanaonya kuna hatari kwamba mrithi wa Rais Kenyatta ataachana na baadhi ya miradi iliyoanzishwa na serikali ya Jubilee, hivyo kuwasababishia Wakenya hasara ya mabilioni ya fedha.

Ripoti ya Kamati ya Bunge kuhusu Bajeti iliyotolewa Juni 2021, ilionyesha kuwa Rais Kenyatta aliachana na mingi ya miradi iliyoanzishwa na serikali ya mtangulizi wake Mwai Kibaki.

Kamati hiyo ilifichua kuwa jumla ya miradi 4,000 ya thamani ya Sh9 trilioni iliyoanzishwa na serikali ya Mzee Kibaki na ya Rais Kenyatta, imekwama au haijakamilika.

Nayo miradi 522 ya Sh1 trilioni imekwama kabisa.Ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa Juni mwaka huu ilisema kuwa mingi ya miradi ya Rais Kenyatta iliyokwama ilizinduliwa kabla ya uchaguzi wa 2017 kwa lengo la kujipatia kura, na haikuwa imetengewa fedha katika bajeti, hivyo ilipuuzwa mara baada yake kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.

MIRADI YA KISIASA

Mtaalamu wa masuala ya kiuchumi George Mboya anasema kuwa miradi mingi ya Rais Kenyatta huenda ikatelekezwa na mrithi wake.

“Miradi mingi huanzishwa kutokana na sababu za kisiasa na wala si kunufaisha watu. Hivyo, miradi ile haitamfaa mrithi wa Rais Kenyatta huenda ikapuuzwa,” anasema Bw Mboya.

Rais Kenyatta pia atamwachia mrithi wake mzigo wa mfumo wa elimu ya CBC ambayo ingali inakanganya Wakenya.

Mfumo huo ulianzishwa mnamo 2017.

Serikali imeanza mchakato wa kujenga madarasa 10,000 yatakayotumiwa na wanafunzi wa sekondari ya chini kuanzia 2023 baada ya Rais Kenyatta kuondoka.

Serikali ijayo pia ndiyo itatwikwa jukumu la kuweka maandalizi ya kuanzishwa kwa mfumo wa CBC katika vyuo vikuu kuanzia 2029.

Mzigo wa madeni pia utakuwa changamoto kubwa kwa mrithi wa Rais Kenyatta.

Afisi ya Bajeti Bungeni (PBO) wiki iliyopita ilisema kuwa serikali inalenga kukopa Sh1.1 trilioni kufikia Juni 2022.

Hatua hiyo itafanya deni la kitaifa kufikia Sh8.8 trilioni. Fedha zinazotumika kulipa madeni kila mwaka zitaongezeka kutoka Sh765.9 bilioni hadi Sh1.36 trilioni.

Rais Kenyatta alipotwaa hatamu za uongozi kutoka kwa Mzee Kibaki deni la kitaifa lilikuwa Sh1.8 trilioni.

Hiyo inamaanisha kwamba Rais Kenyatta amekuwa akikopa Sh1.9 bilioni kwa siku tangu alipoingia mamlakani.

Rais Kenyatta ambaye amesalia na chini ya siku 240 kabla ya mrithi wake kutangazwa, pia ataacha mzigo mzito wa Ajenda Nne Kuu.

Rais wa tano wa Kenya pia atakuwa na kibarua kigumu kupunguza gharama ya maisha ambayo imepanda kwa kiasi kikubwa chini ya utawala wa Rais Kenyatta, kupambana na ufisadi na kubuni mazingira mwafaka kuwezesha mamilioni ya Wakenya wasio na kazi kupata ajira.

Changamoto nyingine itakuwa ni kurejesha heshima kwa maamuzi ya mahakama na utawala wa kisheria.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending