Connect with us

General News

Msako kusitishwa ni nafasi ya kutafuta stakabadhi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Msako kusitishwa ni nafasi ya kutafuta stakabadhi – Taifa Leo

TAHARIRI: Boda: Msako kusitishwa ni nafasi ya kutafuta stakabadhi

NA MHARIRI

IDARA ya polisi jana Jumamosi ilisitisha msako mkali kwa wahudumu wa bodaboda, msako ambao ulitangazwa na Rais Uhuru Kenyatta mapema wiki jana.

Rais aliamuru msako huo baada ya kundi la wanabodaboda, kumdhulumu na kumwibia simu mwanamke afisa wa ubalozi katika barabara ya Wangari Maathai, Nairobi.

Ilisadifu kwamba kitendo hicho kilitokea siku kabla ya maadhimisho ya siku ya wanawake ulimwenguni na kupelekea kulaaniwa vikali na viongozi, wanaharakati na Wakenya kwa jumula wakiwalaumu wahudumu wa bodaboda kwa kuchukua sheria mkononi.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i aliapa kutekeleza mageuzi makubwa katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwataka waendeshaji pikipiki kusajiliwa upya na idara husika.

Jana Jumamosi polisi, kupitia taarifa walisema kwamba msako huo utasitishwa kwa muda ili kuruhusu mazungumzo.

Ieleweke kwamba wanabodaboda wanapaswa kujihimu kujisajili na kuhakikisha kwamba wana leseni za kuendesha pikipiki zao ili wasisumbuliwe na polisi.

Kusitishwa kwa msako hakuna maana kuwa sasa wataendelea kuvunja sheria wapendavyo.

Idara husika zapaswa kuwachukulia hatua kali tena iwapo hawatatahadhari.

Wale ambao pikipiki zao zimekamatwa wanapaswa kuonyesha kwamba wao ndio wamiliki halali wazo na wawe tayari wana stakabadhi stahiki ili warejeshewe, na wanaporejeshewa, wasaini kwamba watazingatia sheria za trafiki ipasavyo kama watu wengine.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending