Connect with us

General News

Mshambuliaji Hakim Ziyech atupwa nje ya kikosi kitakachotegemewa na Morocco kwenye AFCON – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mshambuliaji Hakim Ziyech atupwa nje ya kikosi kitakachotegemewa na Morocco kwenye AFCON – Taifa Leo

Mshambuliaji Hakim Ziyech atupwa nje ya kikosi kitakachotegemewa na Morocco kwenye AFCON

Na MASHIRIKA

FOWADI Hakim Ziyech wa Chelsea ametemwa katika kikosi kitakachotegemewa na Morocco kwenye fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zitakazoandaliwa nchini Cameroon kati ya Januari 9 na Februari 6, 2022.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alikosa mechi zote sita za mwaka huu wa 2021 zilizopigwa na Morocco katika safari ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar. Aidha, hajachezea Morocco almaarufu ‘The Atlas Lions’ tangu aunge kikosi cha kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Burkina Faso mnamo Julai 2021.

 Kocha Vahid Halilhodozic ameteua kiungo Romain Saiss wa Wolves pamoja na Adam Masina na Imran Louza wa Wolves kuwania nafasi ya Ziyech ambayo pia itapiganiwa na Ilias Chair wa Queens Park Rangers (QPR).

Beki Achraf Hakimi wa Paris St-Germain (PSG) pia amejumuishwa katika kikosi cha Morocco ambao wako katika Kundi C pamoja na Ghana, Comoros na Gabon.

Mbali na Ziyech mwanasoka mwingine wa haiba kubwa ambaye ametemwa na kocha Halilhodzic ni beki matata wa Ajax, Noussair Mazraoui.

Kutoitwa kwa Ziyech kambini mwa Morocco ni fahari kubwa kwa Chelsea wanaofukuzia taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel pia kimepangiwa kumenyana na Tottenham Hotspur katika mikondo miwili ya nusu-fainali za Carabao Cup kabla ya kuvaana na Chesterfield katika raundi ya tatu ya Kombe la FA mnamo Januari 8, 2022.

KIKOSI CHA MOROCCO KWA AJILI YA AFCON:

Makipa: Yassine Bounou (Sevilla, Uhispania), Monir El Kajoui, (Hatayspor, Turkey), Anas Zniti (Raja Casablanca, Morocco).

Mabeki: Achraf Hakimi (Paris Saint-Germain, Ufaransa), Sofiane Alakouch (Metz, Ufaransa), Souffian El Karouani (NEC Nijmegen, Uholanzi), Adam Masina (Watford, Uingereza), Sofian Chakla (OH Leuven, Ubelgiji), Samy Mmaee (Ferencvaros, Hungary), Romain Saiss (Wolves, Uingereza), Nayef Aguerd (Rennes, Ufaransa).

Viungo: Aymen Barkok (Eintracht Frankfurt, Ujerumani), Sofyan Amrabat (Fiorentina, Italia), Faycal Fajr (Sivaspor, Uturuki), Azzedine Ounahi (Angers, Ufaransa), Ilias Chair (QPR, Uingereza), Imran Louza (Watford, Uingereza), Selim Amallah (Standard Liege, Ubelgiji).

Mafowadi: Munir El Haddadi (Sevilla, Uhispania), Zakaria Aboukhlal (AZ Alkmaar, Uholanzi), Abdessamad Ezzalzouli (Barcelona, Uhispania), Sofiane Boufal (Angers, Ufaransa), Ryan Mmaee (Ferencvaros, Hungary), Youssef En-Nesyri (Sevilla, Uhispania), Ayoub El Kaabi (Hatayspor, Uturuki).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending