Connect with us

General News

Mshindi wa AFCON nchini Cameroon kutia mfukoni Sh565 milioni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mshindi wa AFCON nchini Cameroon kutia mfukoni Sh565 milioni – Taifa Leo

Mshindi wa AFCON nchini Cameroon kutia mfukoni Sh565 milioni

Na MASHIRIKA

SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF) limefichua kwamba mshindi wa Kombe la Afrika (AFCON) mwaka huu atatia mfukoni kima cha Sh565 milioni, Sh56.5 milioni zaidi kuliko zile ambazo mshindi wa makala ya 32 ya kipute hicho alijizolea mnamo 2019 nchini Misri.

Kikosi kitakachoambulia nafasi ya pili mwaka huu kitaridhika na Sh310.8 milioni huku timu zitakazodenguliwa kwenye hatua za nusu-fainali na robo-fainali zikijizolea Sh248.6 milioni na Sh132.8 milioni mtawalia.

Ina maana kwamba kiasi cha jumla cha fedha ambazo washindi wa mwaka huu kimeongezeka kwa Sh209 milioni zaidi kuliko mwaka wa 2019.

Fainali za AFCON ziling’oa nanga mnamo Januari 9, 2022 nchini Cameroon ambapo wenyeji Cameroon walitandika Burkina Faso 2-1 kabla ya Cape Verde kuwakomoa Ethiopia 1-0 katika mechi mbili za ufunguzi wa Kundi A.

Senegal, Ghana, Ivory Coast na mabingwa mara saba Misri ni miongoni mwa mataifa yanayopigiwa upatu wa kutwaa taji la AFCON nchini Cameroon.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending