Connect with us

General News

Mshukiwa wa mkasa wa moto ulioangamiza watu sita Murang’a kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mshukiwa wa mkasa wa moto ulioangamiza watu sita Murang’a kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi – Taifa Leo

Mshukiwa wa mkasa wa moto ulioangamiza watu sita Murang’a kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi

NA MWANGI MUIRURI

MSHUKIWA mkuu katika mkasa wa moto ambao Jumapili alfajiri uliua watu sita wa familia moja katika Kaunti ya Murang’a sasa atakaa kizuizini kwa siku 21 zaidi ili kusaidia polisi katika uchunguzi.

Hii ni baada ya hakimu Eric Mutunga wa mahakama ya Kandara kutoa idhini hiyo Jumatatu asubuhi baada ya maafisa wa uchunguzi wa jinai (DCI) kutoa ombi hilo.

Bi Alice Nyambura aliyekamatwa Jumapili asubuhi na ambaye hakuhitajika kuitika mashtaka sasa atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kabati hadi Mei 3 ambapo mahakama itatoa maelekezi zaidi.

Katika kisa hicho cha ukatili kilichowaacha wengi vinywa wazi, Bi Mary Wangui Njoroge (60), watoto wake watatu ambao ni Cecilia Gathoni (30), Lucy mumbi (18), Margaret Wanja (15) pamoja na wajukuu wake wawili ambao ni Bi Jackline Wambui (7) na Alvin kiarie (3) waliteketea hadi kuwa jivu.

Mshukiwa ni dadake mdogo wa Bi Njoroge ambao walikuwa wakiishi pamoja katika kijiji cha Nguthuru. Simanzi watu sita wakiangamia ndani ya uhalifu huo wa moto Murang’a.

Maafisa wa DCI tayari wametoa ripoti ya kuonyesha kwamba moto huo ulianza mwendo wa saa saba usiku na ambapo nyumba ya waathiriwa ilikuwa imefungwa kutoka nje, hali ambayo ililemaza juhudu za kuokolewa.

“Mshukiwa tuliye naye mbaroni alikuwa akiishi pamoja na walioaga dunia lakini mnamo Junamosi, akahamisha vitu vyake. Duru zetu za upelelezi zinaashiria kuwa alitoka katika makazi hayo akiwa na tetesi tele za ukorofi. Ametajwa sana na wenyeji kuwa mshukiwa mkuu na ndipo tulimtia mbaroni,” ripoti yao yasema.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa mahakamani na DCI inaelezea kuwa chumbani cha mshukiwa kulipatikana bidhaa za petroli na mishale ya kiberiti inayoashiria kwamba alikuwa ameshiriki kitendo cha uwashaji moto.

Maafisa hao wa DCI wakiomba siku zaidi za kumzuilia mshukiwa walisema kuwa wanahitaji muda zaidi wa kuandikisha taarifa za mashahidi, kupata udadisi wa kimaabara na pia kuandaa ripoti za upasuaji wa miili ili kubaini kiini cha mauti yao.

Seneta wa Murang’a Dkt Irungu Kang’ata alisema kuwa hadi sasa hakuna Sababu za kuridhisha ambazo zimetolewa na vitengo vya kiusalama.

“Hali ya kitamadini ya wakuu wa kiusalama kujitokeza katika mikasa ya ujambazi na kutusimulia jinsi ilifanyika na kwamba maiti zimepelekwa mochari huku uchunguzi ukiendelea ni sawa na kutukejeli. Vitengo vya kiusalama zinafaa kumakinikia hatari za ujambazi kwa njia pana zaidi,” akasema Dkt Kang’ata.

Aliongeza kuwa viongozi wa Kaunti watashirikiana katika kuomboleza na kuandaa maziko, huku akiwataka maafisa wa polisi wasake na watekeleze haki.

Miili ya wote ilipelekwa hadi Mochari ya General Kago mjini Thika kuhifadhiwa huku ikingonja upasuaji wa kitaalamu kubaini hali yao kabla ya kukumbwa na mauti hayo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending