Connect with us

General News

Msiri hadi kifo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Msiri hadi kifo – Taifa Leo

Msiri hadi kifo

NA CHARLES WASONGA

HAYATI Mwai Kibaki aliishi maisha yenye usiri mkubwa kisiasa na kifamilia, tofauti na watangulizi wake Jomo Kenyatta, Daniel Moi na mrithi wake, Rais Uhuru Kenyatta.

Kinyume na Moi na Rais wa kwanza nchini Hayati Mzee Jomo Kenyatta, Kibaki hakuwahi kuandika tawasifu yake kuwaelezea Wakenya kuhusu maisha yake ya kisiasa yaliyodumu kwa miaka 50.

Aidha, hakuna wasifu ambao umeandikwa na watu wengine, kwa idhini yake, kuhusu maisha yake ya kisiasa na kibinafsi.

Hii ni tofauti na mtangulizi wake Hayati Moi ambaye aliidhinishwa kuandikwa kwa wasifu wake, “Moi: Making of an African Statesman”, kilichoandikwa na Andrew Morton. Kitabu hicho kinaangazia utawala wake Moi wake wa miaka 24 na mengi kuhusu maisha yake katika ulingo wa siasa.

Vile vile, Wakenya, na walimwengu kwa ujumla, hawana ufahamu mkubwa kuhusu watoto wa Kibaki, isipokuwa mwanawe wa kwanza Jimmy Kibaki ambaye ameanza kujihususha na siasa.

Mwaka 2021, Jimmy aliteuliwa kuwa naibu kiongozi wa chama cha The New Democrats (TND).

Itakumbukwa kuwa wakati wa urais wake, kati ya 2003 hadi 2013 hayati Kibaki hakuwa na mazoea ya kualika jumbe za wanasiasa na viongozi wa matakaba mbalimbali katika Ikulu ya Nairobi walivyofanya watangulizi wake na hata mrithi wake, Rais Uhuru.

“Ni shughuli rasmi za serikali, kama vile vikao vya mawaziri, ziliendeshwa katika Ikulu ya Nairobi. Rais Kibaki hakupenda kuandaa mikutano yenye maudhui ya kisiasa katika Ikulu,” Bw Matere Keriri mmoja wa marafiki wake wa miaka mingi.

Isitoshe, makazi yake katika mtaa wa Muthaiga na boma lake katika kijiji cha Kanyange, Othaya hayakutembelewa na wanasiasa na marafiki.

Hii ni tofauti na Moi na Jomo Kenyatta ambao walikuwa wakialika wageni katika boma zao Kabarak na Ichwaweri mtawalia.

Bw Keriri anasema kuwa kabla ya kuchaguliwa kuwa rais, Kibaki angetembelea kijiji hicho na kufanya shughuli zake za kibinafsi bila wanajiji kufahamu.

Hii ni tofauti kabisa la mtangulizi wake, Hayati Moi na Rais wa sasa Uhuru Kenyatta ambao walifungua Ikulu kwa mikutano isiyohusiana na shughuli rasmi za serikali na kusalimia watu kokote walikoenda.

Akiongea na wanahabari katika majengo ya bunge Jumatatu, siku ya kwanza kwa umma kuutizama mwili wa babake, Jimmy aliungama kuwa Rais huyo alikuwa mtu ambaye hakupenda kufichua mambo mengi kuhusu maisha yake.

“Katika maisha yake yote kama mwanasiasa, Mzee alikuwa ni mtu ambaye alipenda kulenga maisha yake, majukumu yake serikalini na siasani na masuala ya familia yake,” akasema.

“Hata baada ya kustaafu mnamo 2013 Mzee alijishughulisha zaidi na familia yake, haswa wajukuu wake,” Jimmy akaongeza.

Kutokana na usiri huu, mengi kuhusu maisha ya Hayati Kibaki yatajulikana na kusomwa katika kazi za wandani wake wa kisiasa, watu waliokuwa karibu naye katika utumishi wa umma na watu wachache waliojaribu kuandika kumhusu.

Kwa mfano, sehemu ya maisha ya kisiasa ya Kibaki imeangaziwa katika Wasifu wa kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa jina, “Flames of Freedom”.

Aidha, ameangaziwa katika wasifu za kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, aliyehudumu kama makamu wake katika muhula wake wa pili uongozini, aliyekuwa Mbunge wa Bahari Joe Khamis, aliyekuwa Seneta wa Kitui David Musila na mmoja wa wandani wake marehemu Njenga Karume.

  1. Hakunakili maisha yake ya kisiasa katika vitabu
  2. Hakufungua boma zake na Ikulu kwa jumbe tofauti za wanasiasa walivyofanya watangulizi wake
  3. Angetembea nyumbani kwake kijijini na wakazi wakose kufahamu
  4. Ni machache yanayofahamika kuhusu wanawe isipokuwa Jimmy
  5. Hata kwa marafiki hakupenda kufichua mambo mengi kuhusu maisha yake.
  6. Machache kumhusu yanaangaziwa katika machapisho ya washirika wake serikalini
  7. Hakuwa mtu wa kuzungumzia masaibu yake kisiasa

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending