[ad_1]
Msongamano washuhudiwa kiti cha useneta jijini
NA COLLINS OMULO
IKIWA imesalia miezi miwili kabla vyama kufanya mchujo wa wawaniaji wa viti vya kisiasa kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, kiny’ang’anyiro cha useneta Kaunti ya Nairobi kimezua ushindani mkali kati ya mirengo ya Azimio na UDA.
Katika mrengo wa Azimio, ushindani mkali ni kati ya Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna na mbunge mteule Maina Kamanda.
Mrengo wa UDA nao una wawaniaji wengi huku Milton Lucheri ambaye aliwania kiti cha Westlands mnamo 2017, akiwa wa hivi punde kutangaza kuwa analenga kiti hicho.
Anajiunga na Roy Smith Mwatia maarufu kama Rufftone, Ka – ren Nyamu na George Kamano.
Bw Lucheri alizindua manifesto yake wiki iliyopita katika hoteli moja jijini Nairobi, akiahidi kuwa atawawakilisha vyema wakazi wa jiji kuu na kuhakikisha mgao wa fedha unaongezeka.
Bi Nyamu naye aliwania kiti cha Mwakilishi wa Kike kwenye mchujo wa Jubilee mnamo 2017 na akapoteza kwa Rachel Shebesh.
Kwa upande wake Bw Mwatia anaingia kwenye siasa baada ya kuwa katika sana ya muziki kwa muda wa miaka 20.
Next article
Magavana 3 waahidi Raila kura za ‘zizi’ la Kalonzo
[ad_2]
Source link