[ad_1]
Msusi atoboa siri
Na RICHARD MUNGUTI
MSUSI alishtakiwa Ijumaa kwa kumtandika na kumwumiza msusi mwenzake baada ya mzozo kuhusu mtoto.
William Ochieng Sinoh aliyeshtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Bi Susan Shitubi alitoboa siri kwa kusema : “Mheshimiwa mlalamishi Carolyne Wambui Gathoni ni Msusi mwenzangu na yuko na maneno mengi.”
Akifafanua , Sinoh, alisema , “Wambui amekuwa akidai mimi ndiye baba waq mtoto wake na uwongo mtupu.” Aliendelea kumweleza hakimu , Wambui amekuwa akitisha kumsukuma jela “aozee huko kwa kumchezea.” Akiomba aachiliwe kwa dhamana , Sinoh alimweleza hakimu , kushtakiwa kwake Ijumaa sio mara ya kwanza kukichochewa na Wambui.
Aliomba mahakama imwonee huruma kwa vile anateswa na Wambui kutokana na sababu za kazi. “Tunafanya katika Salon moja na Wambui na kila mara amekuwa akizua vurugu na masengenyo yasiyo na kifani. Niko na watoto wawili mayatima ninaowatunza.Naomba uniachilie kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu,”Sinoh alimsihi hakimu.
Kiongozi wa mashtaka Alice Mathangani hakupinga ombi hilo la mshtakiwa. Lakini Bi Shitubi alimwachilia kwa dhamana ya Sh20,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho. Mbali na dhamana hiyo, hakimu aliagiza idara ya urekebishaji tabia imhoji mshtakiwa ,Wambui pamoja na watu wa familia zao “ndipo ukweli ujulikane.”
Mahakama iliorodhesha kesi hiyo kutajwa Machi 3,2022. “Endapo afisa wa urekebishaji tabia atathibitisha madai yako , nitakuachilia kwa dhamana ya pesa tasilimu,” alisema Bi Shitubi. Sinoh anakabiliwa na shtaka la kumpiga na kumsababishia majeraha Wambui mnamo Januari 26,2022 katika jengo la Diamond Plaza iliyoko Moi Avenue Nairobi.
Mshtakiwa alipelekwa gereza la Viwandani kusubiri akiajiandaa kuwasilisha dhamana.
Next article
Cheruiyot ang’aria wapinzani mita 800 Riadha za AK
[ad_2]
Source link