Connect with us

General News

Mufya yatwaa taji la Patrick Oboya Cup – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mufya yatwaa taji la Patrick Oboya Cup – Taifa Leo

Mufya yatwaa taji la Patrick Oboya Cup

Na JOHN KIMWERE

MUFYA FC imetwaa taji la Patrick Oboya Cup kwa kuzaba Rongai FC mabao 9-8 kupitia penalti baada ya kutoka sare tasa katika fainali iliyopigiwa uwanjani Police Band South B, Nairobi.

Boniface Wambete na Victor Mutuku wa Rongai FC walipoteza penalti zao huku mnyakaji wa MUFYA aliokoa mkwaju uliochanjwa na Ephantus Mungai wa Rongai FC.

Wachezaji wa pande zote walionyesha mechi huku wakishindwa kutumia vyema nafasi walizopata ndani ya kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kocha wa Rongai, Don Magaro alifanya mabadiliko tatu lakini wapi bahati haikusimama.

Chaly Chole, Reuben Ndino na Joseph Wesonga walishuka dimbani kujaza nafasi za Dave Lumumba, Moses Mwangi na Douglas Omunga.

Kwa mara nyingine pande zote zilishindwa kutumia vyema nafasi zilizopata.

”Bila shaka tumekubali yaishe kamwe mchezo huo haukuwa mteremko,” kocha wa Rongaio alisema.

Rongai ilitwaa tiketi ya kushiriki fainali ilipocharaza South B United Sports Academy (SUSA) mabao 2-0.

Nayo Ping FC iliyopigiwa chapuo kutenda kweli na kubeba taji hilo ililala kwa mabao 2-0 mbele ya MUFYA.

Kwenye robo fainali, Rongai FC ilifunga Derby FC mabao 2-0, South B United Sports Academy (SUSA) ilizaba Mariakani Christian Centre (MCC) mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare bao 1-1.

Kwenye robo fainali, Rongai FC ilifunga Derby FC mabao 2-0. PICHA | JOHN KIMWERE

Nayo Ping FC ilisajili ushindi wa bao 1-0 mbele ya Cheza Sports.