Connect with us

General News

Muturi akataa stakabadhi zilizodai Ruto ni mnyakuzi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Muturi akataa stakabadhi zilizodai Ruto ni mnyakuzi – Taifa Leo

Muturi akataa stakabadhi zilizodai Ruto ni mnyakuzi

CHARLES WASONGA na SAMUEL OWINO

SPIKA wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi ametupilia mbali stakabadhi zilizowasilishwa bungeni na Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Wajir, Fatuma Gedi kuhusu madai kuwa Naibu Rais William Ruto ni mnyakuzi wa ardhi.

Bw Muturi alisema stakabadhi hizo hazikuwa halali na hazijatoa ithibati zozote kuhimili madai ya Bi Gedi.

“Badala yake Mheshimiwa Gedi alijaribu kujadili mienendo ya Naibu Rais kinyume cha kanuni za bunge hili. Kwa hivyo naamuru karani wa bunge kuondoa stakabadhi hizo kutoka kwenye rekodi za bunge na azirejeshe kwa Bi Gedi haraka iwezekanavyo,” Bw Muturi akasema.

Mnamo Aprili, Bi Gedi alizua sokomoko bungeni alipodai kuwa Dkt Ruto alinyakua ardhi ya Shule ya Msingi ya Lang’ata na vipande vingine vya ardhi katika kaunti za Narok na Trans Nzoia.

Aliahidi kuwasilisha stakabadhi kuthibitisha madai hayo.Alipofika bungeni Aprili 7, Bi Gedi aliwasili bunge akiwa na mkoba uliojaa stakabadhi alizodai zilikuwa ni ushahidi kuhusu madai yake.