Connect with us

General News

Muturi atetea MCAs kuhusu digrii – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Muturi atetea MCAs kuhusu digrii – Taifa Leo

Muturi atetea MCAs kuhusu digrii

Na KNA

SPIKA wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, ameunga uamuzi wa Mahakama kwamba, wagombeaji udiwani hawahitaji kuwa na digrii.

Bw Muturi alisema suala kuhusu viwango vya elimu hitajika kwa wagombeaji wa nyadhifa mbalimbali lafaa kuamuliwa na mpiga kura. Alitoa kauli hiyo Alhamisi alipolihutubia Bunge la Kaunti ya Bomet Kulingana na uamuzi huo uliotolewa Oktoba 15, 2021, hitaji hilo la Sheria ya Uchaguzi, 2011 ni kinyume cha Katiba.

Mahakama ilisema hitaji hilo la kimasomo kwa wagombeaji linawanyima nafasi watu kufurahia haki ya kikatiba kwa mujibu wa kipengele cha 38 cha katiba.Bw Muturi alisema anaamini kuwa suala hilo limesuluhishwa kwa manufaa ya demokrasia shirikishi.

Alisema Bunge la Kitaifa huajiri wataalamu katika nyanja mbalimbali akitaja wataalamu wa masuala ya uchumi ambao hutoa ushauri kwa Kamati za Bunge kuhusu Fedha na Bajeti, kuhusu masuala kadha ya kifedha.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending