Connect with us

General News

Mvuvi aishtaki serikali kwa kukamata wenzake kiholela – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mvuvi aishtaki serikali kwa kukamata wenzake kiholela – Taifa Leo

Mvuvi aishtaki serikali kwa kukamata wenzake kiholela

NA PHILIP MUYANGA

MVUVI mmoja ameishtaki serikali akipinga kukamatwa kila wakati kwa wavuvi ambao wanajihusisha na uvuvi wa kitamaduni katika maeneo tofauti ya pwani humu nchini.

Bw Mahamoud Abdalla Ali anataka agizo la mahakama kutolewa kuzuia shirika la Kenya Fisheries Service pamoja na maafisa wa polisi na wale wa kikosi cha Kenya Coast Guard kuwakamata wavuvi hao na kutwaa vifaa vyao vya uvuvi.

Katika kesi aliyoiwasilisha katika mahakama kuu Mombasa, Bw Ali alisema kuwa uvuvi wa kitamaduni wa kukidhi mahitaji ya kila siku umekuwa ni nguzo muhimu ya maisha kwa wakazi wa kaunti za pwani.

Kando na Kenya Fisheries Service, Bw Ali pia ameshtaki Kenya Fisheries Advisory Council, Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na mashirika pamoja na mwanasheria mkuu.

Anasema kuwa Kenya Fisheries Service pamoja na maafisa wa polisi wamekuwa wakiwakamata wavuvi wanaotumia njia za kitamaduni za uvuvi na kutwaa vifaa vyao vya kuvua samaki kwa kukiuka sheria ya uvuvi na usimamizi na maendeleo.

Kulingana na stakabadhi za kesi, mtindo wa kutekeleza sheria hiyo unaumiza kipato kidogo cha jamii ya wavuvi wa kitamaduni katika kaunti za pwani na inaathiri uchumi na kiwango cha maisha ya jamii hizo.

“Sheria hiyo ilipitishwa bila kuhusishwa kwa wananchi pamoja na elimu ya raia, pia vipengele vya sheria hiyo vinaathiri uhuru wao, mali, riziki na viwango vya kuishi,” alisema Bw Ali.

Bw Ali alisema kuwa mahakama kuu ya Nairobi kupitia kesi iliyowasilishwa mwaka wa 2012 ilisema kuwa uvuvi ndio kitega uchumi kikuu cha jamii za pwani, na kwamba ulikuwa ni wa kitamaduni.Pia iliamuru kuwa wavuvi wapewe vifaa vya kisasa vya kuvua samaki na idara ya uvuvi.

“Serikali ya kitaifa kupitia idara ya uvuvi, Kenya Fisheries Service na serikali za kaunti hazijawapatia wavuvi wajihusishao na uvuvi wa kitamaduni vifaa vya kisasa vya uvuvi,” baadhi ya stakabadhi za kesi zinasema.

Jaji John Mativo aliagiza kesi hiyo kutajwa mnamo Januari 25 ili maagizo kuihusu kupeanwa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending