Connect with us

General News

Mwalimu kortini kwa kudai kinara wa TSC amefariki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwalimu kortini kwa kudai kinara wa TSC amefariki – Taifa Leo

Mwalimu kortini kwa kudai kinara wa TSC amefariki

Na RICHARD MUNGUTI

MWALIMU wa shule ya msingi alishtakiwa Jumatatu kwa kutuma habari za uwongo katika mtandao wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC), akidai afisa mkuu wa tume hiyo, Dkt Nancy Macharia, amefariki.

Bw Jeremiah Mwawuganga alikabiliwa na mashtaka mawili aliyokana kuhusiana na madai hayo.

Bw Mwawuganga, ambaye ni mwalimu wa shule iliyopo Kaunti ya Makueni, alikanusha mashtaka dhidi yake aliposhtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu katika mahakama ya Milimani, Bi Susan Shitubi.

Mashtaka dhidi ya Bw Mwawuganga yalisema kuwa mnamo Januari 16, 2022, akiwa na nia ya kumsababishia Dkt Macharia pamoja na familia yake dhiki, alichapisha katika akaunti ya TSC kwenye mtandao wa Facebook, kwamba Dkt Macharia ameaga dunia.

Shtaka la pili lilisema mshtakiwa alisambaza katika mtandao wa Facebook wa TSC habari za uwongo Mwalimu huyo alikana mashtaka na kuomba mahakama imwachilie kwa dhamana.

Upande wa mashtaka haukupinga mshtakiwa kuwachiliwa kwa dhamana.

Bi Shitubi alimwagiza mshtakiwa alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh100,000 ndipo aachiliwe kutoka korokoroni.

Kesi hiyo itatajwa Februari 8, 2022.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending