Connect with us

General News

Mwalimu, mshairi na mlezi wa vipaji – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwalimu, mshairi na mlezi wa vipaji – Taifa Leo

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu, mshairi na mlezi wa vipaji

Na CHRIS ADUNGO

KUFAULU kwa mwanafunzi yeyote hutegemea pakubwa mtazamo wa mwalimu wake.

Mwalimu hana budi kuwa na mtazamo chanya anapofundisha wanafunzi ambao bila shaka kiwango chao cha kuelewa mambo hutofautiana.

Ualimu ni zaidi ya kuwasilisha somo darasani! Mwalimu ni mzazi wa wanafunzi wote, rafiki wa karibu, mlezi wa vipaji, daktari wa darasani na mshauri wa maisha anayefaa kuwa mfano wa kuigwa.

“Siri ya kuwa mwalimu bora ni kuwa kielelezo chema kwa hao wadogo wako. Utawezaje kuhimiza wanafunzi kuwa bora ikiwa kauli yako ni ile ya ‘bora wapite mtihani’? Elimu ni zaidi ya

Kupasi mtihani! Mwalimu sharti awe na bidii na wa kwanza kutaka kujifunza na apende kusoma vitabu kwa nia ya kujiimarisha,”anasema Dennis Shonko ambaye sasa ni mwalimu katika Shule ya Msingi ya Entashata, Kaunti ya Kajiado.

Zaidi ya kuwa mwalimu, Shonko ni mwanateknolojia, mshairi shupavu na mwandishi chipukizi. Alizaliwa katika Kaunti ya Narok zaidi ya miaka thelathini iliyopita. Ndiye mwanambee katika familia ya watoto watano wa Bw Joshua Shonko na Bi Emily Shonko.

Alianza masomo katika Shule ya Msingi ya Kwihota, Ruiru, Kaunti ya Kiambu. Akiwa darasa la nane, alijiunga na Shule ya Msingi ya Ilkirragarien, Narok. Alifaulu vyema na akajiunga na Shule ya Upili ya Olololulung’a, Narok.

Huko ndiko alikokutana na Bw Charles Wairegi (Mwalimu Mkuu) na Bi Caroline Wekesa waliompokeza malezi bora ya kiakademia na kumvuvia hamu ya kukichapukia Kiswahili.

Baada ya masomo ya sekondari, Shonko alijiunga na Chuo cha Smart Media, Naivasha kusomea Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

“Ninapenda kutumia maarifa yangu ya kiteknolojia katika ufundishaji. Hufurahi sana ninapowaona wanafunzi wangu wakielewa yote ninayowafunza kwa namna hii. Vifaa vya kidijitali ni muhimu sana katika ufundishaji na ujifunzaji hasa wakati huu ambapo tuna Mtalaa wa Umilisi (CBC),” anakiri.

Mnamo 2014, baada ya kufanya vibarua vya sampuli mbalimbali, Shonko alijiunga na Chuo cha Mafunzo ya Ualimu cha Murang’a hadi mwaka wa 2016. Alitangamana kwa karibu waliokuwa wahadhiri wake, hasa Bw Mose, Bw Nyangweso na Bi Mogambi waliompa ilhamu na kariha zaidi ya kukithamini Kiswahili.

Msukumo wa kutaka kujiendeleza kitaaluma ni miongoni mwa sababu zilizomchochea kujiunga na Chuo Kikuu cha Kenyatta mnamo 2019 anakosomea ualimu hadi sasa.

Baada ya kuhitimu kutoka Murang’a TTC, Shonko alianza kufundisha katika Shule ya Msingi ya Pink Roses, Kiambu. Alihudumu huko kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuguria Shule ya Msingi ya Ridgesview, Naivasha alikoendeleza ari ya kuthaminiwa kwa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi.

Tume ya Huduma kwa walimu (TSC) ilimwajiri Shonko mnamo Januari 2020 na kumtuma kufundisha katika Shule ya Msingi ya Entashata, Kajiado.

Zaidi ya kuandaa miswada mingi ya riwaya, tamthilia, hadithi za watoto na hadithi fupi, Shonko anajivunia pia kuchangia pakubwa safu za mashairi katika gazeti hili la Taifa Leo.

Amekuwa katika safari ya kukuza vipawa vya wanafunzi katika uandishi wa kazi bunilizi tangu afyatue tamthilia ‘Wimbi la Mabadiliko’ iliyochapishwa na kampuni ya Radean Publishers mnamo 2021.D

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending